Uhamisho
wa Paul Pogba kutoka Juventus kuelekea Manchester United uliovunja
rekodi ya dunia sasa unachunguzwa na shirikisho la soka duniani Fifa.
Fifa imeandika barua kwa klabu hiyo ya ligi ya Uingereza ikitaka maelezo zaidi.
Shirikisho hilo linataka kujua ni
nani aliyeshirikishwa katika uhamisho huo wa kitita cha paund milioni
89.3 na ni fedha ngapi zilizolipwa.
Msemaji
wa klabu ya Manchester United :Hatuzungumzii kuhusu kandarasi za watu
binafsi.Fifa imekuwa na nakala hizo tangu uhamisho huo ufanyike mwezi
Agosti.
Pogba anahudumia msimu wake wa
pili katika uwanja wa Old Trafford, baada ya kuondoka katika klaabu hiyo
na kuelekea Juventus kwa kitita cha paund milioni 1.5 mwaka 2012.
Raia huyo wa Ufaransa mara ya kwanza alijiunga na United kutoka klabu ya Ufaransa ya Le Havre 2009 kwa hali ya utata.
Alirudi katika klabu hiyo msimu uliopita kwa kitita kilichovunja rekodi cha Euro milioni 105. Manchester United pia ilikubali kuilipa
Juventus Euro milioni 5 kwa malipo ya ziada pamoja na gharama nyengine
iwapo Pogba atatia saini kandarasi mpya.
Wakati walipothibitisha uhamisho
huo, Juventus ilisema kuwa uhamisho huo umeimarisha uchumi wa klabu hiyo
na kufikia Euro milioni 72.6.
EmoticonEmoticon