Washambuliaji Abdulrahman Mussa
wa Ruvu Shooting na Simon Msuva wa Yanga wameibuka wafungaji bora kwenye
Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa 2016/2017 iliyomalizika Mei 20 mwaka huu.
Kutokana na wachezaji hao
kuibuka vinara kwa ufungaji ambapo kila mmoja amefunga mabao 14,
watagawana zawadi ya mfungaji bora ambayo ni sh. 5,800,000.
Yanga imemaliza Ligi hiyo ikiwa
bingwa kwa ponti 68 na kufunga jumla ya mabao 57, wakati Ruvu Shooting
iliyomaliza katika nafasi ya saba kwa ponti 36 imepachika jumla ya mabao
28.
Watakabidhiwa zawadi hiyo katika
hafla ya tuzo za Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu wa
2016/2017 itakayofanyika keshokutwa (Mei 24 mwaka huu) kwenye ukumbi wa
Mlimani City jijini Dar es Salaam.
IMETOLEWA NA BODI YA LIGI KUU TANZANIA
EmoticonEmoticon