Msanii wa filamu Vicent Kigosi ‘Ray’ amedai kuyumba kwa tasnia ya filamu ni hali ambayo inaweza kuikumba tasnia yoyote.
Muigizaji huyo ambaye anafanya vizuri na
filamu ‘Gate Keeper’ amedai hali hiyo itaondolewa na wasanii hao kwa
kufanya kazi kwa bidii.
“Tasnia ya filamu haijafa kama baadhi ya
watu wanavyodai bali imeyumba na kuyumba ni kitu cha kawaida kabisa kwa
binadamu kwani anaweza kuanguka na akasimama tena,” Ray Kigosi aliiambia
Bongo5.
Anasema kwa hali hiyo wao kama
watayarishaji wakubwa wamekaa kimya wakijipanga na kuendeleza harakati
ambazo zitainua tena soko lao na filamu kurudi katika ubora wao kama
zamani pamoja na changamoto zinazojitokeza kwao ni kipindi cha mpito tu.
“Lazima tasnia itarudi kama awali, ni
sawa tu na maisha ya mtu asiyekata tamaa katika kutafuta anapopata
changamoto anajipanga na kurudi tena na sisi itakuwa hivyo tutarudi kama
awali,” anasema.
EmoticonEmoticon