Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea hati ya utambulisho ya mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini.
Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi.
Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 16, mwaka huu kwa timu 24 zilizogawanywa katika makundi matatu yenye timu nane kila kundi.
Tayari
TFF, ilikwisha kutangaza makundi ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) kwa
timu 24 zitakazochuana msimu huu wa 2017/18 kuwania nafasi tatu muhimu
za kupanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) msimu
wa 2018/19.
Kwa
mujibu wa makundi hayo yaliyoratibiwa na Bodi ya Ligi ya TFF, kundi ‘A’
litakuwa na timu za African Lyon, Ashati United, Friends Rangers za Dar
es Salaam, JKT Ruvu na Kiluvya United za Pwani, Mgambo JKT ya Tanga,
Mvuvumwa ya Kigoma na Polisi Moro ya Morogoro.
Kundi
‘B’ zitakuwa timu za itakuwa na timu za Coastal Union ya Tanga; JKT
Mlale ya Ruvuma; KMC ya Dar es Salam, Mawezi Market ya Morogoro, Mbeya
Kwanza ya Mbeya, Mufundi United ya Iringa, Mshikamano na Polisi Dar za
Dar es Salaam.
Kundi
‘C’ ina timu za Alliance School, Pamba na Toto African za Mwanza, Rihno
Rangers ya Tabora, Polisi Mara ya Mara, Polisi Dodoma ya Dodoma,
Transit Camp ya Shinyanga na JKT Oljoro ya Arusha.
Kadhalika,
TFF imeagiza timu za Ashanti United, Friends Rangers, KMC na Polisi Dar
ya Dar es Salaam kuwasilisha majina ya viwanja vitakavyotumiwa na timu
zao wakati wa ligi hiyo inayotarajiwa kuanza baadaye mwezi ujao.
Kutaja
viwanja hivyo ni matakwa ya Kanuni ya 6 (1) za kanuni Mama ya VPL
inayozungumzia Viwanja kadhalika kusomwa pamoja na Kanuni ya 11
inayozungumzia Leseni za Klabu kwamba kila timu haina budi kuwa na
viwanja vya mcehi za nyumbani ikiwa ni masharti ya kupata leseni ya
klabu.
EmoticonEmoticon