Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameagiza msanii Emmanuel Elibariki anayejulikana kama Nay wa mitego kuachiliwa huru ma wimbo wake wa WAPO uliofungiwa leo na BASATA uchezwe katika vyombo vyote vya habari.
Rais amesema kuwa amefurahishwa na wimbo huo wa ‘WAPO’ na kumshauri msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile wakwepa kodi, wauza unga, wabwia unga, wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili katika jamii.
Akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameishauri Jeshi la Polisi kumuachia huru msanii Nay wa mitego aliyekuwa ameshikiliwa na jeshi hilo.
Waziri Dkt, Mwakyembe amewataka BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.
Hapa chini ni wimbo wa Nay wa Mitego ‘WAPO’ ambao Rais Magufuli ameruhusu uendelee kuchwezwa katika vituo vya redio.
EmoticonEmoticon