Thursday, 27 July 2017

WANAWAKE:- Kwanini mwanaume anaweza kukukataza kufanya baadhi ya vitu? sababu ziko hapa.

WANAWAKE:- Kwanini mwanaume anaweza kukukataza kufanya baadhi ya vitu? sababu ziko hapa.



Mwanaume anaweza kuja na kukuambia “Sitaki uonane na mtu fulani…au sitaki uwe unaenda sehemu fulani…au sitaki ufanye kitu fulani.. au sitaki uwasiliane na mtu fulani.... sitaki urafiki wako na fulani...!” Akamaliza bila kukupa sababu yoyote ile ya kutokufanya hivyo sasa jifanye kiburi kufanya hilo jambo. Hili ni jambo ambalo huwasumbua wanawake wengi.

Ile hali ya kutakiwa kuomba ruhusa kufanya baadhi ya mambo au kuwa na baadhi ya marafiki wakati wanaume wanafanya tu bila kuomba ruhusa. Sitaki kulizungumzia hilo kwa leo ila nataka nikueleweshe ni kwanini wanaume wanafanya hivyo ili hata kama yeye hajakuambia angalau uwe na mwanga kwani unaweza kujikuta unaachika kwa kitu kidogo.


Kimsingi kuna sababu nyingi za kufanya hivyo kwa wanaume ila leo tuangalie sababu kuu tatu za mwanaume kukukataza kufanya kitu fulani au kuongozana na kuwa rafiki na mtu fulani. Sababu hizo ni:-


1. Tabia za yule mtu anayekukataza au madhara ya kile kitu anachokukataza. 



Inawezekana amegundua tabia za hovyo za huyo rafiki yako au huyo mtu na yeye kama mumeo au mwanaume wako hataki ujifunze kutoka kwa huyo mtu na mara nyingi hii ndiyo huwa sababu kubwa.

Mwanaume anaweza kumuona rafiki yako baa anawanaume, akagundua rafiki yako anatembea na mume wa mtu, au ana tabia ya ajabu ambayo haipendi akakukataza kuwa karibu naye. Sasa kinachotokea ni hivi wewe utataka maelezo ya kwanini, lakini wanaume tulivyo si watu wa majungu au kupenda kuongea mambo ya watu.

Hivyo hawezi kukuambia tabia za rafiki yako bali atakukataza tu kuwa karibu naye na kama wewe unajua tabia za rafiki yako mumeo akikukataza jua kashagundua hivyo kaa mbali naye. Lakini pia katika kufanya kitu fulani au kwenda sehemu fulani hii pia inaweza kuwa sababu kwamba amegundua ubaya wa kile kitu au pale mahali na hataki ujihusishe nako.


2. Sababu ya pili ni mwanaume kuwa mwanaume. 


Yaani anaweza kukuambia akiwa hana hata sababu yoyote lakini kwakuwa ni mwanaume na anahisi huyo rafiki anakutia kiburi au kwenda sehemu au kufanya kitu fulani kunakutia kiburi au hapendi tu akakuambia kudhihirisha uanaume wake kuwa amekukataza au akakukataza kwa kukupima tu utii wako kwake au jinsi gani unaweza kumsikiliza kwa mambo ya kuamrisha yeye kama mwanaume. Hapa dada zetu mtuelewe tu kuwa hii kitu ni ya kibaiolojia namna tulivyoumbwa na hata kwenye utii toka enzi na enzi wanaume kutiiwa ni msingi japo.
Hata kwa wanyama, Simba hunguruma si kwasababu ana sababu ya kunguruma bali kuonyesha uanaume wake hivyo mumeo wakati mwingine bila sababu tu ili ujue yeye ni mwanaume anaweza kukuambia hata sitaki uende pahala fulani ni wewe au sitaki usuke, sasa ni wewe kuchagua uende au usuke ili uchague kati ya kwenda au kusuka na ndoa au mahusiano kipi kina thamani zaidi kwako.

3. Sababu ya tatu na hii ndiyo ambayo wanawake wengi hudhani ni kubwa ingawa ni ndogo sana ni kwakuwa labda huyo mtu anayajua madhambi yake hivyo hataki uwe naye karibu kwani anahofu atakuambia. 


Kwamba mumeo anachepuka au anatabia fulani ambayo huyo rafiki yako kaigundua hivyo anajaribu kukuweka mbali na huyo rafiki au sehemu anayofanyia uchafu wake.

Lakini hii si sababu kubwa sana kwani anajua kuwa kama ni kukuambia atakuambia tu, sana sana hapa atatafuta namna ya kukufanya usimuamini huyo rafiki yako akikuambia mambo yake. Sasa ufanye nini unapokutana na hali hii? Wanawake wengi wakiambiwa hivyo huanza na swali “Kwanini?”

Ni kweli ni lazima ujue lakini ni mara chache sana mwanaume atakuambia hasa kama sababu ni ya pili na tatu kwamba anaonyesha uanaume wake au anataka kuficha madudu yake hawezi kukuambia ukweli. Kama ni sababu ya kwanza kwamba rafiki yako ni mchafu atakuambia tu “Sitaki yule rafiki yako ana tabia mbaya!” Ni mara chache sana atakuambia hizo tabia zake mbaya.

Sasa kabla ya kuonyesha kiburi na kuendelea na kitu alichokukataza unapaswa ujiulize “Je huyo rafiki au hiki alichonikataza kina faida kubwa kuliko ndoa yangu..” Lakini pia ujiulize swali la pili “Hivi huyu rafiki yangu akikatazwa na mumewe kuongozana na mimi atamsikiliza mumewe au ataendeleza urafiki?”
Kama huyo rafiki yako ana thamani kuliko mume wako basi endelea na kuongozana naye na kama ni kinyume chake basi achana naye kabisa. Labda nikuambie kitu kimoja, wewe unaweza kuona ni kitu kidogo na ukadhani mwanaume hawezi kukuacha kwakutokutii amri ya kipuuzi kama hiyo lakini kwa mwanaume ni kitu kikubwa.

Kwake kumkatalia ni sawa na kumuondolea uanaume wake, kwamba anaweza kukuambia kitu na ukakataa kufanya halafu bado akakuita mkewe. Kikwetu tunasema “umemkalia mwanaume” hana sauti juu yako na kama hujamlisha ‘limbwata’ jua ni ngumu kukuvumilia.

Anaweza asikuche hapohapo, akajifanya kusahau kabisa kua alikukataza na ukakaidi lakini ukawa ndiyo mwanzo wa kutafuta mchepuko. Wanaume tuko hivi ili kuwa mwanaume ni lazima kuwe na mwanamke anayekusikiliza ambaye unaweza kumpa amri, kama hayupo basi wewe si mwanaume.

Ndiyo ilivyo ndiyo tulivyoumbwa na haiwezi kubadilishwa kwa mikutano mia mbili beijin sijui na sheria. Kama ambavyo mwanamke unahitaji kubembelezwa na kudekezwa hata kama ukiwa raisi ndiyo hivyo wanaume tunahitaji kuwa na nguvu na kuonyesha uanaume wetu.




Ndiyo maana wanaume hupenda wanawake waliowazidi umri, elimu na kipato ili wawe wanaume. Sasa wewe ukitaka kubishana unamuondolea uanaume wake. Hivyo kabla hujakataa bila kujali sababu yake ebu jiulize kama huyo rafiki yako au hicho anachokukataza kina thamani kuliko ndoa yako?

Kama jibu ni hapana achana nacho kama kina thamani basi endelea nacho na mpotezee mume. Kuna mambo ya kubishana na kutaka sababu ya msingi, labda kama hataki ufanye kazi shemu flani, hataki ukasome, hataki ufanye biashara flani na vitu vya maana kama hivyo.

Hapo utajaribu kumshawishi ili akusikilize na mnaweza kufikishana mbali, ila kama kakukataza kuongozana na rafiki ambaye juzi tu kafumaniwa na mume wa mtu halafu bado unamshawishi akuruhusu basi jua unaelekea kuvunja ndoa yako, wanaume huamini kua kama rafiki yako ana tabia flani basi nirahisi na wewe kujifunza tabia hizo.

Labda unaweza kuuliza mbona mimi nikimkataza hanisikii, wanaume tuko hivi, huamini kua sisi tunaweza kufanya maamuzi kuhusu miili yetu kuliko wanaume, kwamba hata kama rafiki yake ni mzinzi anaweza kujizuia na si mwanamke, kwa kiasi flani imani hii ina ukweli. 



Mwanamke anaweza kuchepuka kwa kudanganyika kwa vitu vya kijinga, anaweza kuchepuka kwa kulazimishwa na mazingira kutokana na watu alionao na sehemu na hata ni rahisi kubakwa, lakini mwanaume huchepuka kwa maamuzi bila kujali aina ya marafiki au mazingira aliyopo. Kua makini mumeo anapokukataza kitu kama hakikuathiri kiuchumi au kiafya achana nacho.


EmoticonEmoticon