Thursday, 20 July 2017

Yanga: Kamati ya Wajumbe watatu ya Utendaji Yanga Yatangazwa.

UONGOZI wa Yanga umeteua wajumbe watatu wa Kamati ya Utendaji kujaza nafasi zilizoachwa wazi na waliojiuzulu.
Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface aliwataja walioteuliwa kuwa ni Mohamed Nyenge, Tonny Mark na Majid Suleiman. Alisema mabadiliko hayo ni kwa mujibu wa katiba ibara ya 28:(1)d na maazimio ya kikao cha Kamati ya Utendaji Julai 15. Waliteuliwa na kikao kilichoongozwa na Kaimu Mwenyekiti, Clement Sanga.

Wanachukua nafasi za wajumbe wawili waliojiuzulu na aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano, Mhandisi Malume aliyeenda nje ya nchi kwa masomo ya juu. Mkwasa alisema uongozi wa Yanga pia ulifanya kikao na wachezaji wa zamani wa timu hiyo na kufikia maazimio mbalimbali kuisaidia timu yao na kushirikiana nao.

Wamekubaliana kuwashirikisha masuala ya klabu, kuwa karibu na uongozi, kujenga umoja wa wana Yanga, kuunda safu ya uongozi itakayorahisisha mawasiliano nao. Mengine ni kuweka kumbukumbu kwa ajili ya historia ya klabu na vizazi vijavyo kupitia wao na kusaidiana kuibua vipaji vipya vya wachezaji kwa manufaa yao.


EmoticonEmoticon