Mshambuliaji mpya wa Simba John Bocco, yupo tayari kuirudisha Simba
kwenye mafanikio iliyokuwa nayo siku za nyuma akiwa na Joseph Omog.
Mshambuliaji Mpya wa Simba John Bocco, ‘Adebayor’ amesema chini ya
kocha Joseph Omog, anamatumaini makubwa ya kufanya vizuri na kuipa
mafanikio timu hiyo.
Kwa mara ya kwanza tangu afukuzwe kwenye kikosi cha Azam miaka miwili
iliyopita, Omog, alikutana na Bocco, na kumfundisha mbinu kadhaa za
kutumia ili aweze kufanya vizuri kwenye msimu unaotarajia kuanza hivi
karibuni.
Bocco amesema anajisikia faraja kufanya kazi kwa mara nyingine na
kocha Omog, kwa sababu ni kocha anayemjua vizuri na anaamini msimu ujao
utakuwa na mafanikio kwake na timu ya Simba.
“Nakumbuka msimu wa kwanza kufanya kazi na Omog tulichukua ubingwa wa
Ligi Kuu pale Azam na ninaamini hata msimu ujao nikiwa hapa Simba chini
ya Omog tutafanya vizuri na kutwaa ubingwa,” alisema Bocco.
Mshambuliaji huyo aliyekabidhiwa jezi namba 22, amesema yeye pamona
na wachezaji wenzake wamejipanga kurudisha mafanikio ya Simba ambayo
yamepotea siku za karibuni na kwa ari waliyokuwa nayo hakuna
kitakachoshindikana.
Amesema wanatambua nini ambacho mashabiki na viongozi wao
wanakihitaji msimu ujao hivyo wanajifua kuhakikisha wanakata kiu yao kwa
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu na kufanya vizuri kwenye michuano mingine
watakayoshiriki mwakani.
Bocco ni mmoja wa wachezaji wanne waliosajiliwa na Simba kutoka
kikosi cha Azam wengine ni Shomari Kapombe kipa Aishi Manula na Erasto
Nyoni.
EmoticonEmoticon