Saturday, 22 July 2017

Mbwana Ally Samatta amtunishia kifua Rooney na kuendelea kung’ara barani Ulaya.

NYOTA  na mshambuliaji wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ameendelea kung’ara barani Ulaya, baada ya leo kuifungia timu yake, Genk katika sare ya 1-1 na Everton ya England katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Luminus Arena mjini Genk, Ubelgiji.




Nahodha wa Taifa Stars, Samatta aliifungia Genk bao la kusawazisha dakika ya 55 baada ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney kuanza kuifungia Toffees dakika ya 45.

Huo unakuwa mchezo wa 63 kwa Samatta tangu asajiliwe Genk Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC, akiwa kufunga mabao 24.

Ikumbukwe katika msimu wake wa kwanza, Samatta
alikabidhiwa jezi namba 77, lakini baada ya kazi nzuri, msimu huu amebadilishiwa jezi na kukabidhiwa namba 10.




EmoticonEmoticon