KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Yanga, George Lwandamina amesema wiki
moja inatosha kukinoa kikosi chake tayari kwa ajili ya mechi ya Ngao ya
Jamii Agosti 23 Uwanja wa Taifa.
Pia Lwandamina alisema jana Dar es Salaam wiki moja inamtosha kuandaa
kikosi chake kwa msimu mpya wa ligi na Ligi Kuu ya Tanzania Bara ambayo
imepangwa kuanza Agosti 26 mwaka huu.
Programu ya Lwandamina ilianza kwa mazoezi ya wachezaji kutanua
misuli ya miili kwa wiki moja katika Gym City Mall. Juzi wachezaji
waliingia hatua ya pili ya mazoezi ya uwanjani kufundishwa vitu
mbalimbali ikiwemo mbinu na mifumo.
Alisema kitu alichopanga kuanza nacho ni kutengeneza mfumo wa
uchezaji ambao ni muhimu kuipa timu matokeo mazuri. Alisema
ataiunganisha timu kiuchezaji kwani baadhi ya wachezaji ni wageni hivyo
wanatakiwa kuelewana na msimu uliopita.
Yanga leo wanaenda Morogoro kupiga kambi ya wiki moja kujiandaa dhidi
ya Simba mechi ya Ngao ya Jamii Agosti 23. Katika kujiimarisha zaidi
jana wamemsajili kipa wa Serengeti boys, Ramadhan Kabwili ambaye
ataungana na makipa wengine wawili.
Watacheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida United Agosti 6 Uwanja
wa Taifa. Msemaji wa Yanga, Dismas Ten alisema Lwandamina amepania
kuweka rekodi hivyo anahitaji mazingira yaliyotulia. Simba wako Afrika
Kusini kujiandaa na msimu tangu wiki iliyopita.
EmoticonEmoticon