- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 11 WILAYANI ILEMELA.
- MTOTO AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUKAMATWA NA KULIWA NA FISI WILAYANI KWIMBA.
KWAMBA TAREHE 24.07.2017 MAJIRA YA SAA
05:00HRS ALFAJIRI KATIKA MTAA WA KABANGAJA KATA YA BUGOGWA WILAYA YA
ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MAKUSUDI RASHIDI MIAKA 39, MKAZI WA MTAA
WA IBANGAJA, ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA
BINTI WA MIAKA 11, JINA TUNALIHIFADHI, MWANAFUNZI, NA KUMSABABISHIA
MAUMIVU MAKALI SEHEMU ZAKE ZA SIRI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
AWALI INADAIWA KUWA ALFAJIRI YA MAJIRA
TAJWA HAPO JUU WAZAZI WA MAJERUHI ALIYEBAKWA WALIONDOKA NA KWENDA
KUTAFUTA RIZIKI YA WATOTO HUKU NYUMBANI WAKIWAACHA MAJERUHI NA MDOGO
WAKE WAKIWA WAMELALA. INASEMEKANA KUWA WAKATI MAJERUHI AKIWA AMELALA NA
MDOGO WAKE, GHAFLA ALISTUKA NA KUMUONA MTUHUMIWA TAJWA HAPO JUU AKIWA
ANAMBAKA KWA NGUVU HUKU AKISIKIA MAUMIVU MAKALI NA KUPELEKEA KUPIGA
KELELE ZA YOWE AKIOMBA MSAADA, INADAIWA KUWA BAADA YA MTUHUMIWA KUONA
HALI HIYO ALITOKA NJE NA KUANZA KUKIMBIA.
WANANCHI WALIFIKA KWA HARAKA ENEO LA TUKIO
KUTOA MSAADA AMBAPO BAADA YA KUFIKA WALIMUONA MTUHUMIWA AKIWA
ANAKIMBIA NA KUANZA KUKIMBIZA HADI WALIFANIKIWA KUMKAMATA KISHA WAKATOA
TAARIFA KITUO CHA POLISI, ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA JUU YA
TAARIFA HIZO HADI ENEO LA TUKIO NA KUMKUTA MTUHUMIWA AKIWA CHINI YA
ULINZI WA WANANCHI.
POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA
PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MAJERUHI
TAYARI AMEPELEKWA HOSPITALI KUPATIWA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA
VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU
KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA
WA MWANZA HUSUSANI WAZAZI/ WALEZI AKIWAOMBA KUWA NA MAKAZI SALAMA
YATAKAYOWEZA KUWALINDA WATOTO NA MALI DHIDI YA WAHALIFU. AIDHA PIA
ANAWATAKA WANANCHI WA MWANZA KUWA WAANGALIFU NA MAKINI WAKATI WOTE NA
WATU WENYE NIA OVU DHIDI YA WATOTO.
KATIKA TUKIO LA PILI;
MNAMO TAREHE 23.07.2017 MAJIRA YA 19:00HRS
KATIKA KITONGOJI CHA IZIZIMBA KIJIJI CHA IZIZIMBA “A” KATA YA MHANDE
TARAFA YA MWAMASHIMBA WILAYA YA KWIMBA MKOA WA MWANZA, MTOTO WA KIKE
ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA LIMI BUNZAMA, MIAKA 04, MKAZI WA KIJIJI CHA
IZIZIMBA “A”, AMEFARIKI DUNIA BAADA YA KUKAMATWA NA FISI WAKATI AKIWA
ANACHEZA NA BAADAE KULIWA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HADI KUFARIKI
DUNIA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA NA MAMA
YAKE NJE YA NYUMBA YAO AKIWA ANACHEZA HUKU WAKIWA WANASUBIRI CHAKULA CHA
USIKU. INASEMEKANA KUWA WAKATI MAREHEMU AKIWA ANACHEZA MBALI KIGODO NA
ALIPO MAMA YAKE GHAFLA ALIFIKA MNYAMA FISI NA KUMKAMATA KISHA KUKIMBIA
NAE VICHAKANI. WAZAZI/ MAMA WA
MAREHEMU ALISIKIA KELELE ZA MTOTO WAKE AKILIA NDIPO ALIANZA KUMFUATILIA HUKU AKIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA.
INASEMEKANA KUWA WATU /MAJIRANI WALIFIKA
ENEO LA TUKIO NA KUSHIRIKIANA NA WAZAZI WA MAREHEMU KUMFUATILIA FISI
HUYO, LAKINI KWA BAHATI MBAYA WALICHELEWA KWANI WALIKUTA TAYARI FISI
AMEMUUA MTOTO NA KUMLA SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE KISHA KUKIMBIA
KICHAKANI. AIDHA MABAKI YA MWILI WA MAREHEMU TAYARI YAMEFANYIWA
UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA
MAZISHI, CHANZO CHA KIFO HICHO NI UZEMBE WA WAZAZI KUTOKUWA MAKINI NA
MTOTO, JUHUDI ZA KUMTAFUTA FISI HUYO ILI ASIENDELEE KULETA MADHARA KWA
WATU NA WATOTO KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI BADO ZINAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU
KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA MKOA WA
MWANZA HUSUSANI WAZAZI NA WALEZI AKIWATAKA KUWA WAANGALIFU NA MAKINI
WAKATI WOTE NA WATOTO, ILI KUWAEPUSHA NA AJALI AU NA VIFO VINAVYOWEZA
KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
EmoticonEmoticon