Sunday, 26 March 2017

Wanajeshi 40 Wavamiwa na kuuwawa Nchini Kongo.


Takribani  askari 40 wameuawa katika jimbo la kasai - Jamhuri ya Demokrasia ya Congo na wanamgambo wa waasi wa kikundi cha Kamwina Nsapu.

Askari Polisi 40 wameuwawa na vikosi vya waasi katika jimbo la Kasai nchini Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo

Takribani polisi 40 wameuawa katika jimbo la kasai - Jamuhuri ya Demokrasia ya Cong na vikosi vya waasi wa kikundi cha Kamwina Nsapu.

Kikundi hicho cha waasi kilishambulia msafara wa magari ya polisi waliokua wanasafiri kutoka mji wa Tshikapa kuelekea mji wa Kananga ikiwa ni kulipiza kisasi baada ya waasi hao kushambuliwa vibaya na polisi wa nchi hiyo siku ya ijumaa.

Kikundi cha Kamwina Nsapu kimefanya mauaji hayo huku kikiwaachia polisi ambao walikuwa wanazungumza lugha yao.

Tangu agost mwaka jana kumekuwa na maasahmbulio ya mara kwa mara baina ya vikosi vya usalama vya nchini hiyo ,baada ya askari wa nchi hiyo kumuua kiongozi wa kundi lao ambalo Kamwina Nsapu.

Kwa mujibu wa umoja wa mataifa zaidi ya watu 400 wameuawa kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo huku vikosi kazi vya kutoa msaada vikilaani vikali matumizi ya jeshi kutumia nguvu kubwa kupambana na wanamgambo hao wa waasi.

 ya pamoja ambapo waliouawa katika machafuko hayo walizikwa.

Makaburi 10 yamepatika kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao waliuawa katika mapigano hayo. Pia, kuna maeneo saba ambapo inafikiriwa kuwa nia makaburi.

Wataalamu wawili wa Umoja wa Mataifa, walitekwa nyara wiki mbili zilizopita katika sehemu hiyo ya machafuko.

Hali hiyo ya wasiwasi inaikabili DR Congo muda mrefu sasa.,


EmoticonEmoticon