Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa Timu ya Simba, Haji Manara amefunguka na kusema kuwa mwaka huu lazima Simba itachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara na kuvunja utamaduni wa Yanga kuchukua kombe hilo mfululizo.
Haji Manara amesema hayo leo wakati wa hafla ya kukabidhi jezi na vifaa vya michezo kwa timu zitakazoshiriki Ligi Kuu Bara 2017/2018 iliyoandaliwa na mdhamini Mkuu wa Ligi Kuu Bara.
Mbali na hilo Manara aliomba fedha ziwe zinawaishwa kidogo ili kuweza kusaidia vilabu vingine vidogo ambavyo vinachangamoto kubwa ya mapato ili kusaidia vilabu hivyo kufanya maandalizi kwa wakati.
"Tuangalie hizi timu za mikoani zinapata changamoto nyingi sana tuombe pesa zitoke kwa wakati ili timu ziweza kupanga bajeti zao za usafiri na mambo mengine lakini niseme tu mwaka huu Simba lazima ishinde ubingwa wa Ligi Kuu Bara 2017/2018" alisema Haji Manara
Klabu ya Simba imeshindwa kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa misimu minne sasa huku watani wao wa jadi Yanga wakichukua ubingwa huo mara tatu mfululizo, hivyo kama Simba mwaka huu itashinda inaweza kuvunja mwiko wa Yanga kuchukua ubingwa mfululizo.
EmoticonEmoticon