Kadi nyekundu ya mshambuliaji wa Kagera Sugar Mbarak Yusufu imefutwa na sasa yupo huru kucheza mechi ya mwisho dhidi ya Azam FC Mei 20, 2017.
Bofya hapa kwa habari za michezo zaidi.
Wakati Mbaraka akiruhusiwa kucheza mchezo ujao, mwamuzi aliyechezesha mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar ,Ngole Mwangole ameondoshwa kwenye orodha ya waamuzi wa ligi kuu.
Ngole Mwangole mwamuzi bora wa Ligi Kuu msimu uliopita, alimuonyesha kadi nyekundu ya moja kwa moja Mbaraka Yusuph katika mchezo ulioishia kwa Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2- 1.
EmoticonEmoticon