Wednesday, 17 May 2017

MWANZA: Mti Uliyogoma kung'olewa jijnini humo Na kutoa sauti Umeshaondolewa.


Mti uliowaacha na mshangao mkubwa watu mbalimbali wa Jijini Mwanza kwa kudaiwa kutoa sauti kama binadamu ukipinga kung’olewa, tayari umeshaondolewa katika eneo ulipokuwa kupisha upanuzi wa barabara. 

Mti huo unadaiwa kutoa sauti hiyo jana jioni katika Barabara ya Pasiansi Mwanza wakati uking’olewa kupisha upanuzi wa barabara inayokwenda uwanja wa ndege jijini Mwanza. 

Soma hapa: Ray Kigosi: Tasnia ya filamu haijafa kama baadhi ya watu wanavyodai bali.

Baada ya taarifa hizo kusambaa, watu mbalimbali leo walikusanyika kwenye eneo hilo kuushuhudia mti huo, huko mafundi wa barabara wakiendelea na jitihada za kuung’oa.

Watu wengi waliokuwapo katika eneo hilo, na walioshuhudia tukio hilo jana, walilihusisha na imani ya kishirikina kwani jambo la kawaida kusikia mti ukizungumza 


EmoticonEmoticon