Wakati mchakato wa kugombea uraisi nchini Rwanda, wagombea wa viti vya urais katika uchaguzi utakaofanyika
mwezi wa 8 wanazidi kujitokeza. Diane Rwigara ametangaza rasmi nia yake
ya kugombea urais.
Mwanadada
Diane Rwigara, ametangaza azma yake ya kuwania Urais nchini Nchini
Rwanda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.
Huyu
ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara
aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha .
Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.
Amesema,
kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine
kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha, na kwamba huwezi kusema uko
katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine
wakikimbia nchi.
Huyu
ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza rasmi nia ya kutaka kugombea urais
nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana Mpayimana Philippe aliyetangaza
kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green.
EmoticonEmoticon