Wadau
wa Maendeleo mkoani Mwanza wameidhinisha mikakati mbalimbali ikiwemo
kufanya sensa ya watoto wafanyakazi wa nyumbani na utungwaji wa sheria
ndogo ndogo za kuwalinda watoto, lengo likiwa ni kusaidia mapambano
dhidi ya ukatili kwa watoto hao.
Wamefikia
makubaliano hayo leo kwenye kilele cha mafunzo ya siku tatu kwa
viongozi wa serikali za mitaa kutoka Wilaya za Nyamagana na Ilemela
yaliyoandaliwa na Shirika la kutetea Haki za watoto wafanyakazi wa
nyumbani la WOTESAWA lililopo Jijini Mwanza.
Akizungumzia
mikakati hiyo, Jackline Ngalo ambaye ni Mwanasheria wa shirika la
WOTESAWA amebainisha kwamba, mikakati hiyo itasaidia kuwalinda watoto
wafanyakazi wa nyumbani ikiwemo kuwanusuru na utumikishwaji wa kazi
nzito huku wakilipwa ujira mdogo.
Wadau
walioafiki mikakati hiyo ni Madiwani, Watendaji wa Kata, Wenyeviti wa
Mitaa, Maafisa Ustawi na Maendeleo ya Jamii ambapo wameongeza kwamba
mafunzo hayo yatawasaidia kuielimisha jamii kupitia mikutano ya hadhara
ili kuepukana na ukatili kwa watoto hususani wafanyakazi wa nyumbani.
Baadhi
ya watoto wamekuwa wakikosa fursa ya kusoma kutokana na kuajiriwa
katika kazi za nyumbani kinyume na sheria huku wakilipwa ujira mdogo
tofauti na waraka wamishahara wa mwaka 2013 unavyoelekeza.
Waraka
huo unaelekeza kwamba mfanyakazi wa kazi za nyumbani anapaswa kulipwa
kiwango cha chini cha mshahara ambacho ni shingili 150,000 iwapo mwajiri
ni balozi ama mfanyabiashara mkubwa, elfu 80,000 ikiwa mwajiriwa haishi
kwenye nyumba ya mwajiri wake, elfu 40,000 ikiwa mwajiriwa anaishi
kwenye nyumba ya mwajiri wake na shilingi 130,000 ikiwa mwajiri ni raia
wa kigeni.
EmoticonEmoticon