Aina mpya ya vimelea vya ugonjwa wa kisonono au "gono" ambavyo vinahimili dawa(resistant to drugs) zinazotumika kutibu
ugojwa huu imegundulika duniani. Taarifa iliyotolewa na shirika la afya duniani (WHO) hivi karibuni imesema, ugonjwa wa
kisonono unaoathiri mamilioni ya
watu ulimwenguni umeanza kuwa sugu dhidhi ya dawa zinazotumiwa kuutibu na hivyo kuna hatari ya kutoweza kutibika
kabisa.
Shirika la afya duniani limetoa wito kwa serikali na madaktari kuongeza ufuatlijiaji wa aina hii ya kisonono kutokana na
ugonjwa wa kisonono kuwa
na athari nyingi kama mcharuko (inflammation), ugumba, matatizo wakati wa ujauzito na hata vifo vya kina mama
wajawazito.
“Aina
hii mpya ya vimelea vya kisonono vinaonyesha usugu dhidhi ya dawa zote
za antibiotiki tunazotumia dhidhi yake
ikiwemo dawa za jamii ya cephalosporins ambazo ni dawa za mwisho katika
kutibu ugonjwa wa kisonono, “ alisema Dk. Manjula Lusti Narasimhan,
mmoja wa wanasayansi wa shirika la afya duniani katika kitengo cha
magonjwa ya zinaa.
Miaka michache ijayo, aina hii mpya ya kisonono itakuwa sugu dhidhi ya dawa zote ambazo tunazo saizi “aliendelea
kusema Dk. Manjula LustiNarasimhan
wakati wa mahojiano na shirika la habari la The Associated Press kabla WHO haijatangaza rasmi hatua na
mwongozo mpya wa kukabiliana na tishio la aina hii mpya ya kisonono.
Inakisiwa watu milioni 106 ulimwenguni kote huathiriwa na ugonjwa wa kisonono kila mwaka.Ugonjwa wa kisonono pia
huongeza hatari ya kupata maambukizi ya ugonjwa wa Virusi vya Ukimwi (VVU).
“Ugonjwa sugu wa kisonono sio tatizo la bara la Ulaya au Afrika pekee bali ni tatizo la dunia nzima kwa sasa,’”
alinukuliwa akisema Dk. Manjula LustiNarasimhan.
Kwa mara ya kwanza, vimelea sugu vya ugonjwa wa kisonono dhidhi ya dawa aina ya cephalosporins viliripotiwa katika
nchi ya Japan, ikifuatiwa na Uingereza, Hongkong na Norway.
Wanasayansi wanaamini matumizi mabaya ya dawa aina ya antibiotiki pamoja na uwezo wa vimelea vya ugonjwa wa
kisonono kubadilika na kuzoea
mazingira mapya ndio chanzo kikuu cha kutokea kwa ugonjwa sugu wa kisonono na hivyo muda si mrefu ugonjwa huu
utakuwa janga kubwa dunia
nzima kama hatua za haraka hazitachukuliwa. Kuna uwezekano wa vimelea hivi sugu vya kisonono vinasambaa kwa
sasa duniani bila kuweza
kugundulika kutokana na nchi nyingi kutokuwa na ufuatiliaji na utunzaji kumbukumbu mzuri wa wagonjwa wake.
Shirika la afya duniani limesema nchi zinatakiwa kuongeza ufuatiliaji wa wagonjwa wake pamoja na kudhibiti matumizi
holela ya dawa za antibiotiki mpaka pale taarifa kamili za ugonjwa huu zitakapojulikana.
“Elimu
ya masuala ya kujamiana pamoja na matumizi sahihi ya mipira ya kondomu
inahitajika ili kutokomeza kabisa ugonjwa huu sugu wa kisonono.
Hatuwezi kuutokomeza kabisa ugonjwa huu bali tunaweza kuzuia usambaaji
wake,”alisema Dk. Manjula LustiNarasimhan.
Kwa taarifa zaidi za ugonjwa huu.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE YETU YA FB.
BOFYA HAPA KULIKE PAGE YETU YA FB.
EmoticonEmoticon