- WATU 20 WAMEJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI ILIYOTOKEA WILAYANI MISUNGWI.
- MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI WA KIPIGO MJUKUU WAKE NA KUSABABISHA KIFO CHAKE WILAYANI MISUNGWI.
KWAMBA TAREHE 10.05.2017
MAJIRA YA SAA 16:00HRS KATIKA BARABARA YA KIJIJI CHA MWABAKOYE KATA YA
LUBILI TARAFA YA MBARIKA WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, GARI NAMBA
T.793 AINA YA ISUNZU TIPA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA RASHIDI SAIDI @ KASANZU ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI WA MIAKA KATI 30
HADI 35 MKAZI WA GEITA LIKITOKEA KWENYE MACHIMBO YA DHAHABU KWENDA
KUSAGA MAWE YA DHAHABU MAENEO YA ISHOKELAHELA ILIYOPO KATA YA KISESA W
ILAYANI MAGU LILIACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WA
WATU 20 WALIOKUWA WAMEPANDA GARI HILO.
MAJERUHI WA AJALI HIYO
WAMEFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.KHAMIS MANG’OMBE MIAKA 36 MKAZI WA KAHAMA,
2.SAMWEL SELEMAN MIAKA 35 MKAZI WA ISHOKELA, 3.MAYOMBO JOHN MIAKA 23
MKULIMA WA ISHOKELA, 4.WANDU MADUKA MIAKA 32 MKAZI WA ISHOKELA, 5.PETER
SHIGI, 6.JOSEPH BUJIKU, 7.MUSA BUJIKU, 8.MANGU MASALU, 9.JULIUS AMOS,
10.DIGA MAPUYA 11.JOHN MAYOMBO, NA 12. ASHA OMARI MIAKA 47 MKAZI WA
ISHOKELA. AIDHA MAJERUHI SITA BADO MAJINA HAYAKUFAHAMIKA KWANI HALI ZAO
BADO SIO NZURI WAMEKIMBIZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA
MATIBABU, AIDHA KATI YA MAJERUHI TAJWA HAPO JUU WA NNE WAMELAZWA
HOSPITALI YA MKOA YA SEKOU TOURE, MAJERUHI SABA WAMELAZWA HOSPITALI YA
WILAYA YA MISUNGWI NA MAJERUHI MMMOJA AMELAZWA HOSPITALI YA MASASI
MISUNGWI HUKU MAJERUHI WAWILI WAKIRUHUSIWA.
CHANZO CHA AJALI NI UZEMBE WA
DEREVA KUSHINDWA KUJAZA BREKI ZA GARI UPEPO KABLA YA KUANZA SAFARI
KWANI BREKI ZA GARI HILO ZINATUMIA UPEPO HALI ILIYOPELEKEA KUFELI BREKI
WAKATI ALIPOKUA ANAZIKAMATA HALI ILIYOPELEKEA KUPINDUKA, LAKINI PIA GARI
LILIKUWA LIMEBEBA WATU WENGI HUKU LIKIWA LIMEBEBA MAWE KINYUME NA
SHERIA. DEREVA WA GARI HILO AMEKAMATWA YUPO KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA
POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
ANIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA
VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUWA NA UTARATIBU WA KUKAGUA MAGARI YAO KABLA
YA KUANZA SAFARI, LAKINI PIA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA
USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA VIFO NA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
KATIKA TUKIO LA PILI;
KWAMBA TAREHE 10.05.2017 MAJIRA YA
SAA YA SAA 01:00HRS USIKU KATIKA KIJIJI CHA MHUNGWE KATA YA MABUKI
WILAYA YA MISUNGWI MKOA WA MWANZA, MTU MWANAMKE ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA SHIJA MATHIAS MIAKA 55, MKAZI WA KIJIJI CHA MHUNGWE ANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMFANYIA UKATILI MJUKUU WAKE AITWAYE
NGONDA BALANGI MIKA 07 KWA KUMCHAPA FIMBO SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI
WAKE HALI ILIYOPELEKEA BAADAE KUPOTEZA MAISHA.
INADAIWA KUWA MAREHEMU ALICHELEWA
KURUDI NYUMBANI WAKATI ALIPOKWENDA KUCHEZA, AIDHA INADAIWA KUWA WAKATI
ALIPORUDI NYUMBANI KWAO MAJIRA TAJWA HAPO JUU BIBI YAKE ALIMKAMATA KISHA
AKANZA KUMCHAPA FIMBO NYINGI SEHEMU MBALIMBALI ZA MWILI WAKE HALI
ILIYOPEKEA MAREHEMU KUPOTEZA NGUVU NA BAADAE KUFARIKI DUNIA.
MTUHUMIWA WA MAUAJI HAYO YUPO
KATIKA MAHOJIANO NA JESHI LA POLISI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
ATAFIKISHWA MAHAKAMANI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA
NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAZAZI AU WALEZI
AKIWATAKA KUWA NA UTARATIBU WA KUWAFUNDISHA WATOTO MAADILI MAZURI KWA
NJIA YA KAWAIDA NA SIO KWA VIPIGO, KWANI VIPIGO VINAWEZA KUHATARISHA
MAISHA YA MTOTO KISHA KUPELEKEA MZAZI KUINGIA KWENYE MATATIZO.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
EmoticonEmoticon