TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 22.05.2017
WATU WATATU WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI HUKU MWINGINE
MMOJA AKIENDELEA KUTAFUTWA KWA TUHUMA ZA KUMBAKA BINTI MMOJA WILAYANI
ILEMELA.
KWAMBA TAREHE 21/05/2017 MAJIRA YA SAA
19:00HRS KATIKA MAENEO YA MAMLAKA YA PAMBA KATA YA KIRUMBA WILAYA YA
ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATATU WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA
1.FREDY REMIGIUS MIAKA 20, MKAZI WA KITANGIRI, 2.JACKSON JOSEPH MIAKA
17, MKAZI WA MLIMANI B NA 3.FRANK HARUNI MIAKA 18, MKAZI WA MLIMANI B,
HUKU MTUHUMIWA MWENGINE MMOJA AKIENDELEA KUTAFUTWA, WANASHIKILIWA NA
JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA BINTI MMOJA JINA TUNALIHIFADHI
MWENYE UMRI WA MIAKA 15, MKAZI WA KIRUMBA, NA KUMSABABISHIA MAUMIVU
MAKALI SEHEMU ZA SIRI, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.
INADAIWA KUWA BINTI ALIKUWA NA MAHUSIANO
YA KIMAPENZI NA MTUHUMIWA ALIYEJULIKANA KWA JINA MOJA LA PHILI NA MAJIRA
TAJWA HAPO JUU WALIPANGA WAKUTANE MAENEO YA MAMLAKA YA PAMBA,
INASEMEKANA KUWA BINTI ALIKUTANA MPENZI WAKE MAHALI HAPO KISHA
WALIKWENDA SEHEMU YENYE JUMBA BOVU KUZUNGUMZA, WAKIWA KWENYE ENEO HILO
GHAFLA WALITOKEA VIJANA WENGINE WATATU TAJWA HAPO JUU WAKISHIRIKIANA NA
MPENZI WAKE BINTI AITWAYE PHILI NA KUANZA KUMFANYIA UKATILI WA KUMBAKA.
INASEMEKANA KUWA WAKATI WAKIENDELEA NA
UKATILI HUO BINTI ALIPIGA YOWE AKIOMBA MSAADA KUTOKA KWA WANANCHI,
WANANCHI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUMUOKO BINTI NA KUFANIKIWA KUMKAMATA
MTUHUMIWA MMOJA AITWAYE FREDY REMIGIUS KISHA WALITOA TAARIFA POLISI
KUHUSIANA NA TUKIO HILO, ASKARI WALIFIKA ENEO LA TUKIO NA KUFANYA MSAKO
MKALI WA KUWATAFUTA WATUHUMIWA WENGINE HUKU WAKISHIRIKIANA NA WANANCHI
NA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WENGINE WAWILI TAJWA HAPO JUU, HUKU
MMOJA ALIYEKUWA NA MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA BINTI AKIFANIKIWA KUTOROKA.
MSAKO WA KUMTAFUTA MTUHUMIWA ALIYETOROKA
BADO UNAENDELEA, AIDHA POLISI WAPO KATIKA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA
WALIOKAMATWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI,
MAJERUHI ALIYEBAKWA AMEPELEKWA HOSPITALI YA MKOA WA MWANZA SEKOU TOURE
KWA AJILI YA MATIBABU NA HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU
KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA
WA MWANZA AKIWAOMBA KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU/UHALIFU KWA
JESHI LA POLISI HUSUSANI WA VITENDO VYA UBAKAJI ILI WAHALIFU WA AINA HII
WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
EmoticonEmoticon