Monday, 26 June 2017

Salmin Hoza asaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam msimu ujao na kusema haya.

Salmin Hoza amesema anamtihani mkubwa wa kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kurudi kwenye kiwango chake.

Siku chache baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Azam msimu ujao kiungo wa Mbao FC Salmin Hoza amesema anamtihani mkubwa wa kuhakikisha anaisaidia timu hiyo kurudi kwenye kiwango chake.

Hoza ameiambia Goal, hakutegemea kama ipo siku atacheza klabu kubwa kama Azam lakini kwakua imetokea atajitahidi kuweza kupambana ili kutimiza malengo ya timu hiyo msimu ujao.

“Najua kama mimi ni mchezaji mwenye kiwango cha juu lakini sikutegemea kama ningecheza Azam nashukuruku kwa nafasi hii na mimi nimewaahidi kujipanga na kuhakikisha nafanya vizuri katika kipindi chote nitakachokuwa hapa,”amesema Hoza.

 Mheshimiwa Edward Lowasa atakiwa kuripoti mbele ya Mkurugenzi wa makosa ya jinai uchunguzi (DCI)

Kiungo huyo ambaye pia ameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ‘Taifa Stars’ kilichokwenda Afrika Kusini hivi karibuni amesema anafurahi kwa kipaji chake kuonekana akiahidi mashabiki wa Azam kuwa atafanya vizuri.

Hoza amesema  ndoto yake katika soka ni kufika mbali hivyo, anaamini kujiunga na Azam ni hatua kubwa kwake.

“Malengo yangu ni kufika mbali na kitendo cha Azam kutambua kipaji changu naona sasa ni njia zinaanza kufunguka, kwani nahitaji kufanya makubwa zaidi ikiwezekana kutoka hata nje,”amesema.



Hoza ambaye awali alikuwa akiwaniwa na Yanga amesema atatumia uwezo wake wote kwa kushirikiana na wachezaji wenzake kwa ajili ya kuirudisha Azam kwenye michuano ya kimataifa mwaka 2019.



Source: GOAL


EmoticonEmoticon