Friday, 23 June 2017

Hans Pope amethibitisha na kutaja siku ya Okwi kuja SIMBA na kusaini.

Baada ya headlines za muda mrefu kuhusiana na ujio wa mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda Emanuel Okwi kuja kujiunga na Simba kuzidi kuenea, huku mitandao ya kijamii ikiripoti kuwa mchezaji huyo tayari amesaini mkataba na Simba.

BOFYA HAPA KUSOMA RATIBA YA LIGI KUU YA UINGEREZA (EPL) 2017 - 2018.

Kupitia ukurasa wake wa twitter alithibitisha kuwa bado hajasaini mkataba wowote na Simba, hiyo ni baada ya kuenea kwa picha kati yake na mwenyekiti wa kamati ya usajili wa Simba SC Zacharia Hans Pope wakiwa pamoja Kampala.



June 22 Hans Pope amethibitisha kuwa Okwi anakuja Tanzania siku ya Jumamosi ya June 24 na atasaini mkataba wa miaka miwili “Mimi nilituma picha tu kuwa Okwi yupo Kampala lakini nimezungumza nae tumefikia makubaliano na anakuja Jumamosi atasaini mkataba” >>>Hans Pope





EmoticonEmoticon