1. CHOKOCHOKO
Wanaume
wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila
wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi
hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa
kuleta chokochoko, huepukwa.
Ni
vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba
vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake
kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake,
yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.
Mara
nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko,
mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye
mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki
baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa
kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.
2. KUTORIDHIKA
Wanaume
wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata
uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba
hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake,
haridhiki tu.
Anaanza
kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa
fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi
wake ya kufurahia uhusiano wao. Anamfanya kila anapokutana naye awaze
atapigwa mzinga.
Bahati
mbaya sasa kila atakachopewa haridhiki. Anatamani kikubwa zaidi.
Wanaume wengi siku hizi wanaichukia tabia hiyo. Hawapendi kuwa na
mwanamke ambaye haridhiki na kile kidogo walichojaliwa. Wanaume wengi
wakiona hivyo huwa wanaanza kumuepuka mwanamke wa ‘sampuli’ hiyo.
Kwake
kunakuwa hakuna jema. Badala ya kumshauri mpenzi wake mbinu za
kujikwamua kiuchumi yeye ni lawama tu. Kila siku analalamika kwamba
wanaume wengine wanawapa wapenzi wao mahitaji muhimu lakini wa kwake
hamtimizii.
Mwanaume
akiona kila analofanya kwa mpenzi au mkewe haridhiki, hatoi shukurani
ni rahisi kupunguza mapenzi kwa mtu wake. Taratibu anaanza kujitoa na
hata kuhamishia mapenzi kwa mtu mwingine ambaye atakuwa anaridhika kwa
kidogo anachopewa. Ni muhimu kuridhika.
3. KULINGANISHA
Hii
nayo ni tabia isiyopendwa na wanaume wengi. Wanaume wanapenda kuishi
maisha yao. Wanapenda kuheshimiwa na wapenzi wao. Wanapenda kumsikia
mwanamke akisema; ‘hakuna mwanaume mwingine wa kufanana na wewe.’
Mwanaume
anapenda kuhakikishiwa kwamba hakuna mwanaume mwingine kama yeye. Yeye
ndiye mzuri au bora kuliko wanaume wengine hivyo mwanamke anapoanza
kuonesha tabia za kumlimnganisha na mwanaume mwingine linakuwa tatizo
kubwa.
Mwanaume
anakasirika. Anaona ni rahisi mwanamke wake kumtamani mtu mwingine baki
kuliko yeye. Sifa anazozitoa kwa mwanaume mwingine ni nzuri hivyo
zinamvutia. Kama zinamvutia siku yoyote anaweza kushawishika kumfuata
yule anayemvutia.
Wanawake
wanapaswa kuwa makini katika eneo hilo. Hata kama umeona kuna kitu
kizuri kimekuvutia kutoka kwa mwanaume mwingine, kamwe usije kumwambia
mwenzi wako. Baki nalo moyoni. Jipe moyo kwamba mwanaume uliyenaye ndiye
bora kuliko wanaume wote duniani.
4. KUWA TEGEMEZI
Wakati
mwingine hata kama huna kitu lakini mwanamke unashauriwa kutojionesha
huna kitu. Jioneshe kwamba una kitu hata kama huna. Wanaume wa sasa
hawapendi kuwa na mwanamke ambaye kila kitu anategemea kutoka kwa
mwanaume.
Hata
kama huna kazi lakini ni vyema basi mwanamke akajaribu kufanya biashara
ndogondogo ambazo zitampunguzia mwanaume wake makali ya kuombwa fedha
kila wakati. Wanaume wanapenda kuwapa wapenzi wao fedha lakini inapozidi
kipimo inageuka kuwa kero.
Yani
kuanzia mahitaji ya kila siku, saluni, mavazi, ada ya watoto na mengine
mengi mwanamke anamtegemea mwanaume. Yeye hataki kujishughulisha hata
kidogo. Anataka aletewe, kazi yake kubwa ni kulea familia nyumbani.
Mwanaume
akigundua mwanamke ni tegemezi mkiwa katika hatua za mwanzoni, ni
rahisi kumkimbia mwanamke na kwenda kwa mwanamke ambaye angalau atakuwa
hamtegemei kwa kila kitu. Mwanamke anayejiongeza hata kwa kutoa wazo la
kuanzishiwa biashara ambayo itamfanya asiwe tegemezi.
5. KUTOKUA MUELEWA
Mwanaume
anapenda mwanamke muelewa. Hapendi mwanamke mbishi hata kama jambo lipo sahihi na mwanaume wake anataka liwe hivyo ila mwanamke amazidi kuwa mbishi wanaume wanachukia hiyo tabia kutoka kwa wapenzi wao.
Anatamani kuwa na
mwanamke ambaye akimueleza kitu, anajiongeza na kufanya zaidi ya pale
mwanaume alipofikiria. Mwanaume anapenda mwanamke atakayeanzisha wazo la
kimaendeleo na kumshirikisha mpenzi wake ili walifanye.
Wanaume
wanapenda wanawake wanaowaelewa. Kama mwanamke anakuwa si wa kumuelewa
mpenzi wake, kumsaidia basi mara nyingi mwanaume humkimbia.
6. KUJITAPA KWA KUWA NACHO
Hakuna
mwanaume anayependa kutawaliwa. Wanawake wenye fedha mara nyingi
wanakuwa na tabia ya kutaka kuwatawala wanaume. Anataka mwanaume afanye
kile ambacho yeye anataka. Fedha zinamvimbisha kichwa na kuona kwamba
anaweza kuwa na mamlaka ya kumuamrisha mumewe.
Anatumia
fedha zake kama fimbo ya kumchapia mpenzi wake. Ni vigumu sana wanaume
kumvumilia mwanamke wa aina hiyo, mara nyingi wanajiepusha naye. Kwa
kutumia fedha zake anaweza kupata mwanaume mwingine lakini pia
watashindwana katika suala la kumtawala.
7. KUWA BIZE SANA
Wanaume
wengi hawapendi mwanamke tegemezi lakini pia wanaume haohao wanachukia
mwanamke akiwa bize sana na kazi zake. Mwanaume hapendi kuona mwenzi
wake anakuwa bize na kazi au biashara zake kiasi ambacho kitamfanya hata
akose muda na mwenzi wake.
Unachotakiwa
kufanya hapo mwanamke ni kujigawa. Hakikisha unakuwa bize na kazi
lakini si ya kupitiliza maana itamfanya mwanaume akose muda wa kuwa na
wewe pale anapokuhitaji, badala yake anaweza kwenda kwa mwanamke
mwingine ambaye hayupo bize.
EmoticonEmoticon