Wednesday, 7 June 2017

TAARIFA Ya JESHI LA POLISI KUTOKA MKOANI MWANZA

  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUVUNJA USIKU OFISI ZA IDARA YA MAJI WILAYA YA UKEREWE.




  • WATU WA NNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA KOSA LA KUPATIKANA NA MIRUNGI KIASI CHA KILOGRAMU 56.75, WILAYANI NYAMAGANA.


KWAMBA TAREHE 07/06/2017 MAJIRA YA SAA 04:15HRS ALFAJIRI KATIKA MTAA WA BUKONGO WILAYA YA UKEREWE MKAO WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE MISAKO NA DORIA WALIFANIKIWA KUMKAMATA DALIS ATHUMANI @ MTAA WA SABA, MIAKA 27, MKAZI WA KIJIJI CHA BULIMBA AKIWA NA KOKI 68 ZA MAJI, STOPER 04, JOINT ZA KOKI 07, KEY BOARD YA COMPUTER 01, MONITOR 01, CPU 01, NA PRINTER 01, MALI ZA OFISI YA IDARA YA MAJI HALMASHAURI YA WILAYA YA UKEREWE AMBAZO ALIVUNJA NA KUIBA USIKU OFISINI HAPO, KITENDO AMBACHO NI KOSA KISHERIA.


AWALI ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA KATIKA MAENEO YA MJI WA NANSIO – UKEWERE WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA WASIRI KWAMBA KATIKA OFISI ZA IDARA YA MAJI WILAYANI HAPO WAPO MTU/WATU AMBAO WANAFANYA UHALIFU, KUTOKANA NA TAARIFA HIZO BAADHIA ASKARI WALIWEKA MTEGO KATIKA BARABARA ZINAZOELKEA MAENEO HAYO KISHA WENGINE WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA HADI OFISI HAPO, NDIPO BAADAE MTUHUMIWA DALIS ATHUMANI ALIKAMATWA MAENEO YA MTAA WA BUKONGO AKIWA NA VITU TAJWA HAPO JUU MALI ZA OFISI YA IDARA YA MAJI.


POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA MTUHUMIWA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI. AIDHA POLISI WANAENDELEA NA MSAKO PAMOJA NA UPELELEZI WA KUWATAFUTA WATU WENGINE WANAOJIHUSISHA NA MTUHUMIWA KATIKA UHALIFU WILAYANI HAPO.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI  NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI WAMILIKI WA TAASISI ZA SERIKALI NA WATU BINAFSI AKIWATAKA KUWA NA UTARATIBU WA KUWEKA WALINZI KATIKA OFISI ZAO ILI KUWEZA KUWADHIBITI WAHALIFU WA AINA KAMA HII MAPEMA KABLA HAWAJALETA MADHARA KATIKA OFISI ZAO. AIDHA PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUENDELEA KUTOA USHIRIKIANO KWA JESHI LA POLISI KWA KUTOA TAARIFA MAPEMA ZA WAHALIFU NA UHALIFU ILI WAWEZWE KUKAMATWA MAPEMA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA KATIKA TUKIO LA PILI;


MNAMO TAREHE 07/06/2017 MAJIRA YA SAA 05:00HRS ALFAJIRI KATIKA MTAA WA MBUGANI “A” KATA YA MBUGANI WILAYA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, ASKARI WAKIWA KWENYE DORIA NA MISAKO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WA NNE WALIOFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1. THOMAS ZACHARIA, MIAKA 25, MKAZI WA MTAA WA UNGUJA – MWANZA, 2.ALLY ATHUMANI MIAKA 35, MKAZI WA KAHAMA -SHINYANGA, 3.NYAMURYA ELIA, MIAKA 35, MKAZI WA MTAA WA UNGUJA – MWANZA, NA 4.STANSLAUS MAPINDUZI @ ELIAS MIAKA 41, MKAZI WA TARIME, WAKIWA NA MADAWA YA KULEVYA AINA YA MIRUNGI MAFUNGU 57, YENYE KIASI CHA KILOGRAMU 56.75, YAKIWA YAMEMEWEKWA KWENYE MABEGI NA MAGUNIA, KITENDENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.


AWALI ASKARI WAKIWA DORIA NA MISAKO KATIKATI MWA JIJI LA MWANZA WALIPOKEA TAARIFA KUTOKA KWA RAIA WEMA KWAMBA  NYUMBA MOJA ILIYOPO MTAA TAJWA HAPO JUU WAPO WATU WANAOJIHUSISHA NA BIASHARA YA MIRUNGU. AIDHA BAADA YA ASKARI KUPOKEA TAARIFA HIZO WALIANZA KUFANYA UPELELEZI NA UFUATILIAJI HADI MAENEO HAYO, NDIPO MAJIRA TAJWA HAPO JUU ASKARI WALIWEZA KUIBAINI NYUMBA HIYO KISHA ASKARI WALIINGIA NA KUIFANYIA UPEKUZI.


AIDHA NDIPO KATIKA  UPEKUZI HUO ASKARI WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WA NNE TAJWA HAPO HUKU WAKIWA NA KIASI HICHO CHA MIRUNGU. POLISI WAPO KATIKA UPELELEZI NA MAHOJIANO NA WATUHUMIWA WOTE WA NNE, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI.


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAKAZI WA JIJI NA MKOA WA MWANZA HUSUSANI VIJANA AKIWATAKA KUACHA KUJIHUSISHA NA BIASHARA ZA MADAWA YA KULEVYA KWANI NI KOSA KISHERIA NA ENDAPO MTU ATABAINIKA ATAKAMWATWA KISHA ATAFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.


 IMETOLEWA NA:

DCP: AHMED MSANGI


KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA


EmoticonEmoticon