Baada ya kuondoshwa kwenye
michuano ya SportPesa na timu ya daraja la kwanza inayoshiriki nchini
Kenya, uongozi wa timu ya Simba umevunja kambi rasmi na kuamua kuwapa
mapumziko wachezaji kabla ya kurejea kwa mara nyingine kujiwinda na
msimu ujao wa ligi kuu ya Tanzania bara.
Makamu wa rais wa Simba,Geofrey
Nyange Kaburu amesema kuwa mapumziko hayo hayawatahusu viongozi kwani
kwa upande wao bado wanaendelea na mchakato wa usajili na maswala
mbalimbali yanayohusiana na klabu.
Kaburu alisema kwamba kwa sasa
uongozi ushafanikiwa kukamilisha usajili wa wachezaji wawili ambao
ni Jamali Mwambeleko kutoka timu ya Mbao FC pamoja na Yusuf Mlipili toka
Toto African iliyoshuka daraja ambao jana walionekana kwenye kikosi
cha Simba kilichocheza dhidi ya timu ya Nakuru All Stars.
Alisema kwamba hata swala la
mchezaji Emanuel Okwi kama lipo kwenye mapendekezo ya mwalimu basi
uongozi utalifanyia kazi kupitia kamati yake ya usajili inayongozwa na
Zakaria Hans Pop
EmoticonEmoticon