Donald Ngoma inaaminika ameamua kuachana na soka la
Bongo, badala yake anatimkia Afrika Kusini atakapojiunga na Polokwane
alikosaini miaka mitatu.
Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma, akitarajiwa
kuwasili nchini leo kumalizana na ama klabu ya Yanga au mahasimu wao
Simba, mchezaji huyo ni kama anachezea akili za miamba hao wa soka baada
ya taarifa za ndani kudai ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea
timu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.
Ngoma alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuongeza
mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga, lakini pia mshambuliaji huyo
alishafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Simba na inasemekana ujio
wake ilikuwa ni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kwa kusaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Kwa mujibu wa Mtandao wa KickOff.com, imethibitika
Mzimababwe huyo amekamilisha zoezi lake la usajili kwenye klabu hiyo,
baada ya kuwa huru kufuatia kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na
mabingwa wa soka Tanzania Yanga.
Taarifa hiyo imesema Ngoma, alisaini mkataba huo wa miaka mitatu
baada ya kufuzu vipimo vya afya na anatarajiwa kujiunga na miamba hao wa
ligi ya ABSA,ambao kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa
ligi hiyo.
Akiwa Polokwane City, Ngoma anatarajiwa kukutana na Mzimbabwe mwezake
ambaye pia anacheza nafasi ya George Chigova aliyewahi kucheza naye FC
Platinum chini ya kocha Norman Mapeza.
BOFYA HAPA KUJUA VIINGILIO VYA KWENYE MAONYESHO YA UWANJA WA SABASABA MWAKA HUU
BOFYA HAPA KUJUA VIINGILIO VYA KWENYE MAONYESHO YA UWANJA WA SABASABA MWAKA HUU
EmoticonEmoticon