Saturday, 24 June 2017

HIMID Mao amesema hatoweza kujiunga na Yanga kwasababu kuna timu mbili za nje zinamuhitaji.



Mao amesema hatoweza kujiunga na Yanga kwasababu kuna timu mbili za nje zinamuhitaji ambao ni Randers ya Denmark na Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoshiriki michuano ya COSAFA, Himid Mao, amesema hatoweza kujiunga na Yanga kwasababu kuna timu mbili za nje zinamuhitaji ambao ni Randers ya Denmark na Bidvest Wits ya Afrika Kusini.

Himid Mao ameiambia Goal, alikuwa na mpango wa kujiunga na mabingwa hao wa soka Tanzania, lakini amebadilisha mawazo baada ya kupokea hofa hizo mbili.

“Ni timu kubwa na ofa zao ni nzuri hapa namsubiri wakili wangu kuniambia niwapi niweze kwenda ili kujiunga nao ,”amesema Himid Mao.

Mchezaji huyo amesema kwasasa yupo bize na majukumu ya timu ya taifa lakini baada ya kumalizika kwa michuano ya COSAFA, ataweza kuweka wazi ni timu gani atajiunga nazo kati ya hizo mbili.

Amesema anafurahi kuona timu kubwa kama Yanga ikimuhitaji lakini nivyema aende nje ili akatafute changamoto nyingine na maslahi makubwa kwasababu soka ndiyo kazi yake.

“Naishukuru Yanga, kwa kuonyesha kukubali kiwango changu lakini sitoweza kujiunga nayo kwasababu ninaofa nyingine ambayo ninzuri kwangu na kwataifa pia,”amesema.


Yanga walikuwa wakimuhitaji mchezaji huyo kwa ajili ya kuimarisha eneo lao la kiungo lakini kwasasa mpango huo umeharibika baada ya ofa za Randers na Wits ya Afrika Kusini.



Source: Goal


EmoticonEmoticon