Sunday, 9 April 2017

Viingilio kwa mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu KESHO katika Meschi Ya SIMBA SC Vs MBAO FC

Uongozi wa uwanja wa CCM kirumba wa mkoani Mwanza umeweka wazi viingilio kwa mashabiki na wapenzi wa mpira wa miguu wanaotaka kuushuhudia mchezo wa Simba sports Club vs Mbao Fc utakaochezwa siku ya Jumatatu/Kesho katika uwanja huo wa CCM kirumba


Meneja wa uwanja huo Bwana:Steven Shija amesema kuwa upande wa
'VIP'bei itakuwa Tsh 20,000
Kwenye Ngazi itakuwa Tsh 10,000
Mzunguko itakuwa 5,000 tu.

Aidha Shija amewatahadhalisha wapenzi wa soka juu ya watu watakokuwa wakiuza tiketi mitaani kuwa,tiketi za mchezo huo zitapatiana uwanjani tu na si mahala pengine

Kuhusu swala la ulinzi Shija amesema wamejipanga vizuri kwa kushirikiana na jeshi la polisi mkoani hapo kuwa watahakikisha kuwa wanaimarisha ulinzi wa hali ya juu ili kuhakikisha usalama kwa raia watakaokuja kushuhudia pambano hilo


EmoticonEmoticon