Baada ya kukaa kwa mwezi mmoja
nchini Morocco pamoja na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya
wenyeji wa Michuano ya U17 Gabon huku ikipata ushindi wa magoli 2-1
mechi zote kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa jina kama Serengeti
Boys usiku wa kuamkia Leo kimetua salama nchini Cameroon kwa mechi mbili
za kirafiki.
Wakiongozwa na Kocha Mkuu wao
Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ vijana wa Serengeti Boys wataanza mazoezi
kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa wenyeji timu ya vijana ya Cameroon
utakaochezwa kesho siku ya Jumamosi ukiwa ni mchezo wa Maandalizi ya
Michuano ya AFCON kwa vijana inayotarajiwa kutimua vumbi May 14 nchini
Gabon.
Serengeti Boys imekuwa gumzo
barani Afrika na kuanza kutabiriwa kuwa ni timu ambayo inatakiwa
kuchungwa zaidi katika Michuano ya AFCO U17 inayotarajiwa kuanza mwezi
wa tano kutokana na kuonesha upinzani na kuzifunga timu kubwa ambazo
zipo katika michuano hiyo hii ni baada ya kutoka sare na Ghana ya mabao
2-2 mjini Dar es salaam na kugawa dozi kwa wenyeji Gabon mechi zote
mbili kwa ushindi wa maabao 2-1.
Serengeti Boys inakutana na
Cameroon siku ya kesho huku ikiwa na kumbuku ya kufanya vema michezo
yote ya kirafiki huku ikiwa haijawahi hata kupoteza mchezo mmoja wa
kimataifa ukiachana na ule ilipofungwa na Congo-Brazaville katika hatua
ya kutafuta tiketi na baada ya mchezo wa kesho timu hizo zitarudiana
tena siku ya Jumanne.
Serengeti Boys inatarajia kwenda
Gabon kwa ajili ya Michuano hiyo ya AFCON U17 May 7 ambapo Michuano
hiyo itaanza May 14 huku Tanzania ikiwa kundi B na timu za Ethiopia
waliopewa nafasi ya Mali ambao wamefungiwa na FIFA kwa miaka minne
nyingine ni Niger na Angola na Kundi A lina timu za Ghana,Cameroon,Gabon
na Guine na kila kundi litatoa timu mbili ambazo moja kwa moja zitafuzu
Michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17
zitakazofanyika nchini India Novemba mwaka huu.
EmoticonEmoticon