Friday, 14 April 2017

BAADA YA SIMBA KUPEWA POINTI TATU NA TFF KAULI YA YANGA HAPA.



Uongozi wa Yanga umesema hautaenda mahakamani kupinga Simba kupewa pointi tatu.

Simba imeshinda rufaa yake dhidi ya Kagera Sugar na kupata pointi tatu na mabao matatu ikiwa ni baada ya kubainika beki Mohamed Fakhi alicheza mechi dhidi ya Simba akiwa na kadi tatu za njano.

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amesema kama kuna wanachama wanataka kwenda mahakamani, wao hawatakuwa na uwezo wa kuwazuia huku akisisitiza Tanzania ikifungiwa, Serengeti Boys itang’olewa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa Afrika na ile kauli mbio ya Gabon mpaka Kombe la Dunia itageuka na kuwa “Gabon hadi Nyumbani Tanzania”.

“Wakiendelea hivi itakuwa ni Gabon hadi Nyumbani, haitakuwa Kombe la Dunia tena.

”Watu wana hasira zao, sisi viongozi tunaweza tusijue kinachoendelea. Kagera ni timu ndogo, wanaonewa, hawatendewi haki. Sasa sisi tumeinunua hii kesi.

“Ajabu kabisa, waamuzi wameitwa wawili tu na wengine hawakuitwa. Hii si sawa, kuna jambo hapa,” alihoji Mkemi akionekana ni mwenye jazba.


EmoticonEmoticon