Saturday, 29 April 2017

Muzamiru Yassin ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Simba kwa mara ya pili msimu huu, na atapewa ...

Muzamiru Yassin ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Simba kwa mara ya pili msimu huu, na atapewa milioni 5 kama ilivyo desturi.

Klabu ya Simba imemteua kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi kiungo mshambuliaji Mzamiru Yassin baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia Goal  jopo lao la makocha limeamua kumpa tuzo hiyo Mzamiru kwakuwa amecheza kwa kujitoa hata timu yao kuwa hapo ilipo.

“Mwezi Machi ulikuwa ni wa neema kwa Mzamiru alifunga bao moja kwenye mchezo na Kagera Sugar ambako tulifungwa mabao 2-1 na kwenye mechi iliyofuata dhidi ya Mbao alifunga bao la ushindi katika ushindi wa 3-2,” amesema Kaburu.

Kiongozi huyo amesema kama ilivyokuwa kawaida kwa wachezaji wengine Mzamiru atazawadiwa Sh Milioni 5, ambazo zitaongeza hamasa kwa wachezaji wengine wazidi kujituma na kuipa timu yao mafanikio wanayoyahitaji.

Amesema zoezi hilo litaendelea hadi mwishoni mwa msimu na kwa msimu huu limekuwa na mafanikio makubwa kwao kwani viwango vingi vya wachezaji vilipanda kutokana na hamasa hiyo kutoka kwa uongozi.

Kaburu amesema imani yao Mzamiru na wachezaji wengine wa Simba wataitumia vizuri fursa hiyo katika mwezi mmoja uliobaki wa mechi za ligi ili kupata tuzo hiyo ya mwezi Aprili ambayo itakuwa ya mwisho kwa msimu huu wa 2016/17.


Hiyo ni mara ya pili kwa Mzamiru kubeba tuzo hiyo, huku ikiwa ni msimu wa kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.


Bofya hapa kuLike page yetu ya FB

Bofya hapa kwa habari za michezo zaidi.


EmoticonEmoticon