Kocha Mkuu wa timu ya Toto African ya Jijini Mwanza maarufu wanakisha mapanda, Furgence Novatus amesema timu hiyo kamwe haitashuka daraja kutokana na matumaini makubwa ya ushindi kwa mechi nne walizobakiza licha ya kuwa wako katika mstali wa hatari kushuka ligi.
Kocha huyo ametoa tambo zake mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya Toto African na Buselesele FC, mabingwa wapya wa Mkoa wa Geita ligi daraja la tatu, ambapo Novatus amesema hata Mabingwa wa ligi kuu timu ya Yanga hawatawabakisha salama wasipojipanga na kwamba hakuna urafiki katika hatua waliopo.
Baada ya mchezo huo ambao timu hizo zilitoshana nguvu, wadau wa soka Mkoani Geita wamekuwa na matumaini makubwa na timu yao, ambayo iko katika maandalizi ya kuchuana ligi daraja la pili.
Diwani wa kata ya Buselesele Godfrey Miti ambaye ni mdhamini wa Timu ya Buselesele FC amedai kuwa matumaini makubwa aliyonayo ni kuakikisha timu hiyo inafikia kiwango cha ligi kuu na kwamba yeye pamoja na wadau wa mpira Mkoani Geita hataakikisha timu hiyo inapanda daraja.
EmoticonEmoticon