Kikao
cha kamati ya sheria, katiba na hadhi za wachezaji kimeahirishwa mpaka
hapo kitakapo kaa wakati mwingine, huku kwa sasa uamuzi wa kamati ya
Saa 72 uliopa Simba ushindi wa pointi tatu na mabao matatu kufuatia
malalamiko yao dhidi ya Kagera Sugar kumchezesha Mohamed Fakhi kinyume
na kanuni ukiendelea kubakia kama ulivyo.
Siku
ya Alhamisi, Kamati ya Saa 72 ilikaa kikao katika hosteli za TFF na
kufikia uamuzi wa kuipa Simba pointi tatu baada ya kujiridhisha kuwa
Fakhi alicheza pambano la Simba huku akiwa na kadi tatu za njano kinyume
na kanuni.
Kikao
cha leo chini ya mwenyekiti Richard Sinamtwa kilikaa kupitia ombi
Kagera Sugar la mapitio mapya ya hatua zilizopelekea wao kupokwa pointi
tatu.
Utata
ulikuwepo katika kadi ya pili iliyohusisha mechi baina ya Kagera Sugar
na African Lyon. Wakati Fakhi na viongozi wa Kagera Sugar wakisisitiza
kuwa hakuoneshwa kadi, nyaraka za ripoti ya mechi kutoka kwa mwamuzi na
kamisaa zilionesha kuwa alioneshwa kadi dakika ya 72 kwa kosa la
kumrukia mchezaji wa African Lyon.
EmoticonEmoticon