KWAMBA TAREHE 08.04.2017 MAJIRA YA SAA 18:30HRS KATIKA BARABARA YA KENYATA ENEO LA ROUND ABOUT YA SAMAKI KATA NA WILAYA YA NYAMAGANA JIJI NA MKOA WA MWANZA, WATU WATANO WAMEPATA MAJERAHA SEHEMU MBALIMBALI ZA MIILI YAO WALIPOKUWA WAKISAFIRI WAKIWA KWENYE GARI LENYE NAMBA T.377 AUM AINA YA MITSUBISH FUSO LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA AMBAE HAKUFAHAMIKA JINA KWANI ALITOROKA ENEO LA TUKIO, HII NI BAADA YA GARI HILO KUACHA NJIA NA KUPINDUKA.
MAJERUHI WA AJALI HIYO WAMEFAHAMIKA KWA MAJINA YA 1.SHABANI RAMADHANI MIAKA 21, MNYAMWEZI, MAKAZI WA BUTIMBA, AMEUMIA MGUU WA KUSHOTO, 2.BUBELWA ALPHAN MIAKA 24, MHAYA, MKAZI WA BUTIMBA, AMEUMIA MGUU WA KUSHOTO, 3.KULWA ELIKANA MIAKA 20, MHAYA, MKAZI WA BUTIMBA AMEUMIA MGUU WA KULIA, 4.RAZARO NATHANIEL MIAKA 22, MSUKUMA, MKAZI WA BUTIMBA, AMEUMIA MKONO WA KUSHOTO NA 5. HASSAN HABIB MIAKA 27, MHAYA, MKAZI WA BUTIMBA, AMEUMIA KISIGINO CHA KULIA.
INADAIWA KUWA DEREVA WA GARI HILO ALIKUWA KATIKA MWENDO KASI AKITOKEA UWANJA WA NYAMAGANA AKIWA NA ABIRI WACHEZAJI MPIRA WAKIELEKEA BUTIMBA, NDIPO ALIPOFIKA KATIKA ENEO LA ROUND ABOUT YA SAMAKI ALISHINDWA KULIMUDU GARI, KISHA GARI LIKAACHA NJIA NA KUPINDUKA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA WATU TAJWA HAPO JUU AMBAO WALIKUWA ABIRIA WA GARI HILO.
ASKARI POLISI KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI AMBAO WALIKUA KARIBU NA ENEO LA TUKIO WALIFIKA ENEO HILO KWA HARAKA NA KUFANIKIWA KUOKOA MAJERUHI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI, JUHUDI ZA KUMTAFUTA HADI KUMKAMATA DEREVA WA GARI HILO BADO ZINAENDELEA, MAJERUHI WAMELAZWA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI, AIDHA ABIRIA WENGINE AMBAO WALIKUWEPO KWENYE GARI HILO TAYARI WAMECHEKIWA AFYA NA KURUHISIWA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WAENDESHAJI WA VYOMBO VYA MOTO AKIWATAKA KUFUATA SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI PINDI WAWAPO BARABARANI ILI KUEPUSHA AJALI NA VIFO VINAVYOWEZA KUEPUKIKA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
EmoticonEmoticon