NAHODHA Msaidizi wa Klabu Bingwa
ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, ameweka wazi
kuwa wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri kuelekea mchezo wa Kombe
la Shirikisho (Azam Sports Federation Sports) dhidi ya Simba Jumamosi
ijayo.
Kikosi cha Azam FC kipo kwenye
maandalizi makali kuelekea mchezo huo, ambapo tayari kimeshaingia
kambini tokea jana katika makao makuu ya klabu hiyo ndani ya viunga vya
Azam Complex kujiandaa na mchezo.
Himid ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa kikosi hicho kipo vizuri na watanufaika na urejeo wa wachezaji wao muhimu waliokuwa majeruhi.
“Morali iko juu, timu ipo vizuri
bahati nzuri wachezaji wenzetu karibia asilimia 90 wapo vizuri na wapo
fiti na wako tayari kwa mchezo na naamini kocha atakuwa na nafasi nzuri
ya kuchagua timu yake ya kwenda kucheza mchezo huo,” alisema.
Kiungo huyo anayesifika kwa
ukabaji na mwenye mashuti makali, aliongeza kuwa mchezo huo utakuwa
mgumu licha ya kufanikiwa kuwafunga mara mbili katika mechi mbili
zilizopita.
“Usidhani kama mchezo huu wa tatu
utakuwa mrahisi kama mara mbili zilizopita tulizoshinda, kwani Simba
nayo inajipanga, lakini naamini sisi tutajipanga vizuri zaidi ili kuweza
kushinda mechi hiyo inayokuja,” alisema.
Himid ambaye amekulia kwenye timu
hiyo kwa takribani miaka tisa sasa, alitoa wito kwa mashabiki wa Azam FC
kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti kwani wao ni
sehemu muhimu sana katika timu na uwepo wao utawaongezea nguvu zaidi
uwanjani ya kuibuka kidedea.
Bofya hapa kuLike page yetu ya FB
Bofya hapa kwa habari za michezo zaidi.
Bofya hapa kuLike page yetu ya FB
Bofya hapa kwa habari za michezo zaidi.
EmoticonEmoticon