Friday, 30 June 2017

Viungo bora wakabaji kwa msimu uliomalizika wa 2016/2017.

Ni nyota wachache wanaoweza kuimudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara, tangu zipite zama za kina  Selemani Matola, Athumani Idd na wengine ambao walifanikiwa kuimudu nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, sasa eneo hilo limekuwa likitesa klabu nyingi kwenye Ligi kwa kukosa watu sahihi

Kwa msimu uliomalizika wapo baadhi ya wachezaji walifanikiwa kucheza vizuri nafasi ya kiungo mkabaji, kwa asilimia kubwa walitimiza majukumu yao ya kuilinda safu yao ya ulinzi isipate madhara pindi wanapo shambuliwa na kuisukuma timu mbele wakati wakiwa na mpira


Himid Mao ( Azam)

Ndiye kiungo mkabaji bora kwa sasa hapa nchini, anaongoza kwa kupokonya mipira , Himid nyota wa Azam na timu ya taifa Tanzania, amekuwa mzuri kwenye  kuilinda safu yake ya ulinzi isipatwe na madhara kwa kuzuia hatari zote, kiungo huyo amekuwa na nidhamu kubwa kwenye eneo hilo kuliko kiungo yeyote kwa sasa

Jonas Mkude (Simba)

Kiungo huyo amekuwa mzuri kwenye kupiga pasi fupi fupi na ndefu kwa usahihi bila kupoteza, Mkude amekuwa muhimili mkubwa ndani ya Simba katika eneo la katikati hasa la ulinzi na kuifanya timu iwe kwenye usalama pindi ikiwa inashambuliwa mara kwa mara

Shabani Nditi (Mtibwa Sugar)

Licha ya umri wake kuwa mkubwa ila bado nyota huyo alifanikiwa kuhimudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa asilimia kubwa tofauti na matarajio ya wengi, Nditi amekuwa imara kwenye utimamu wa mwili hasa ikitokea kwenye mipira ya kugombania dhidi ya timu pinzani

Kenny Ally (Singida United)

Amejiunga na Singida akitokea Mbeya City aliyoichezea msimu uliopita, Kenny ana sifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali, ni mzuri kwenye kusoma mchezo kwa haraka na kugundua udhaifu na ubora wa mpinzani

Ally Nassoro (kagera Sugar)

Nyota wa klabu ya Kagera amefanikiwa kucheza kwa ubora mkubwa kwenye eneo la kiungo mkabaji kila anapopewa nafasi kwenye eneo hilo, ana uweo wa kupiga pasi fupi na ndefu pia ni mzuri kwenye kukaba bila kufanya faulo hali kadhalika ana uwezo mkubwa wa kufunga, amemaliza na magoli zaidi ya matatu licha ya kucheza chini sana

Stephan Kingue (Azam)

Ukitaja wakata umeme kwenye Ligi msimu uliopita jina la Kingue haliwezi kosekana, alionesha umaridadi wake hasa kwenye mashindano ya Mapinduzi kabla ya kuumia, Kingue siyo mzuri sana kwenye kupiga pasi kama wengine ila ni shapu kwenye kufika kwenye tukio kwa haraka na kulizuia, pia ni mzuri kwenye kuzuia mipira ya juu kutokana na kimo chake.





Read More

The front pages of Newspapers in Tanzania today, June 30, 2017

Read More

Thursday, 29 June 2017

Mchezaji Amis Tambwe Aongeza MKATABA YANGA.

Read More

Baada Donald Ngoma kuongeza mkataba wa kuichezea Yanga.

Baada Donald Ngoma kuongeza mkataba wa kuichezea Yanga, kocha George Lwandamina amesema kitu alichokifanya Ngoma ni cha kupongezwa

Baada ya mshambuliaji Donald Ngoma, kuongeza mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina, amesema kitu alichokifanya Ngoma ni cha kupongezwa.


Lwandamina ameiambia Goal, anamuhitaji sana Ngoma kwenye kikosi chake cha msimu ujao hivyo kitendo cha kuongeza mkataba kimempa matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao.

“Ni jambo zuri na wachezaji wengine wanatakiwa kuiga mfano wake Ngoma ni mchezaji anayestaili kuichezea Yanga kutokana na rekodi yake aliyoifanya akiwa na timu hiyo huko nyuma,”amesema Lwandamina.

Mzambia huyo amesema baada ya kushindwa kumtumia kwa muda mrefu msimu uliopita anaamini msimu ujao atakuwa na nafasi kubwa ya kutimiza majukumu yake uwanjani na kuwafurahisha mashabiki wao.

Amesema kubaki kwa Ngoma kwenye kikosi cha Yanga kutaongeza hofu hata kwa wapinzani wao, na kuendelea kuiogopa timu hiyo msimu ujao.

“Kuwa na Ngoma tunapata uhakika wa kuogopwa na wapinzani wetu kwani wamekuwa wakimuhofia sana hiyo ni faida kwetu ambayo tunapaswa kuitumia vyema kupata pointi tatu,”amesema.

Ngoma amesaini Yanga, mkataba wa miaka miwili, na kuzima uvumi ambao ulikuwa umeenea kuwa yupo mbioni kujiunga na wapinzani wao Simba ambao nao walikuwa wanamuhitaji.

Mzimbabwe huyo ameigarimu Yanga dola 420,000 kwa ajili ya mkataba huo utakaomuweka Jangwani hadi mwishoni mwa msimu wa 2019.
Read More

Wednesday, 28 June 2017

Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF na Katibu Mkuu wake wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Rais wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili kupisha uchunguzi dhidi yao. 


Tukio hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru, Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya kumaliza uchunguzi wao.


Licha ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria.



Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika.

Wengine ni aliyekuwa katibu mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka (FAT sasa TFF), Michael Wambura na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayubu Nyenzi.

Gazeti la Nipashe lilieleza kubaini kuwa, mkutano mkuu wa wanachama wa TFF uliofanyika Desemba 2011 uliidhinisha Kampuni ya Ukaguzi ya TAC kuwa mkaguzi wa hesabu za shirikisho kwa miaka mitano kuanzia mwaka ulioishia Desemba 31, 2011.

Ripoti ya ukaguzi wa kampuni hiyo inaonesha kuwa, katika kipindi cha kuanzia Agosti 15, 2014 hadi Septemba 30, 2015, TFF ililipa jumla ya Sh. milioni 274.072 kwa Wambura na kampuni za Punchlines (T) Ltd na Artriums Dar Hotel Ltd bila kuwa na nyaraka stahiki.

Pia, ripoti ya ukaguzi maalum wa fedha za udhamini wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa timu ya taifa (Taifa Stars) iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inabainisha matumizi mabaya ya mabilioni ya shilingi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa TFF.

Katika ripoti hiyo inaelezwa kuwa, kuanzia Novemba 13, 2013 hadi Februari 15, 2014, jumla ya dola za Marekani 315,577 (sawa na sh. milioni 688.368) zilichotwa kwenye akaunti ya fedha za udhamini wa TBL kwa Taifa Stars na kutumika kinyume cha makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa shirikisho na kampuni hiyo.

Inaelezwa pia kwenye ripoti hiyo kuwa kuanzia Novemba 11, 2013 hadi Machi 11, 2014, jumla ya dola za Marekani 381,248 (Sh. milioni 831.616) zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF.

Miongoni mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia kinyume fedha hizo ni Malinzi, Matandika, Ali Ruvu, Nyenzi, Ally Mayay, Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara, Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.

Ripoti ya ukaguzi wa TAC inaonesha Wambura alilipwa jumla ya Sh. milioni 67.5, Punchline (T) Ltd ililipwa Sh. milioni 147.154 na Artriums Dar Hotel Ltd ililipwa Dola za Marekani 28,027 (Sh. milioni 59.417).

Aidha, ripoti hiyo inaonesha malipo ya maelfu hayo ya Dola kwa Artrium yalifanyika siku moja ya Machi 4, 2015 kwa TFF kuandika vocha nne zenye namba 001467, 001468, 001469 na 001470, tatu zikiidhinisha malipo ya Dola 9,000 kila moja wakati moja ikiidhinisha malipo ya Dola 1,027.

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa timu ya ukaguzi ilibaini malipo kwa wadau hao wa soka yalifanyika bila idhini ya Kamati ya Utendaji ya TFF. 

Read More

Tuesday, 27 June 2017

Donald Ngoma imeaminika ameamua kuachana na soka la Bongo.... Aitema SIMBA NA YANGA.

Donald Ngoma inaaminika ameamua kuachana na soka la Bongo, badala yake anatimkia Afrika Kusini atakapojiunga na Polokwane alikosaini miaka mitatu.


Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma, akitarajiwa kuwasili nchini leo kumalizana na ama klabu ya Yanga au mahasimu wao Simba, mchezaji huyo ni kama anachezea akili za miamba hao wa soka baada ya taarifa za ndani kudai ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea timu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.

Ngoma alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuongeza mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga, lakini pia mshambuliaji huyo alishafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Simba na inasemekana ujio wake ilikuwa ni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kwa kusaini mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo msimu ujao.

Kwa mujibu wa Mtandao wa KickOff.com, imethibitika Mzimababwe huyo amekamilisha zoezi lake la usajili kwenye klabu hiyo, baada ya kuwa huru kufuatia kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na mabingwa wa soka Tanzania Yanga.

Taarifa hiyo imesema Ngoma,  alisaini mkataba huo wa miaka mitatu baada ya kufuzu vipimo vya afya na anatarajiwa kujiunga na miamba hao wa ligi ya ABSA,ambao kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo.


Akiwa Polokwane City, Ngoma anatarajiwa kukutana na Mzimbabwe mwezake ambaye pia anacheza nafasi ya George Chigova aliyewahi kucheza naye FC Platinum chini ya kocha Norman Mapeza.

BOFYA HAPA KUJUA VIINGILIO VYA KWENYE MAONYESHO YA UWANJA WA SABASABA MWAKA HUU
Read More

The front pages of Newspapers in Tanzania today, June 27, 2017

Read More