Sunday, 30 April 2017

The front pages of Newspapers in Tanzania today, APRIL 30,2017.





 


























Read More

Saturday, 29 April 2017

Muzamiru Yassin ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Simba kwa mara ya pili msimu huu, na atapewa ...

Muzamiru Yassin ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Simba kwa mara ya pili msimu huu, na atapewa milioni 5 kama ilivyo desturi.

Klabu ya Simba imemteua kuwa mchezaji bora wa mwezi Machi kiungo mshambuliaji Mzamiru Yassin baada ya kutoa mchango mkubwa kwa timu hiyo.

Makamu Mwenyekiti wa Simba Godfrey Nyange ‘Kaburu’ ameiambia Goal  jopo lao la makocha limeamua kumpa tuzo hiyo Mzamiru kwakuwa amecheza kwa kujitoa hata timu yao kuwa hapo ilipo.

“Mwezi Machi ulikuwa ni wa neema kwa Mzamiru alifunga bao moja kwenye mchezo na Kagera Sugar ambako tulifungwa mabao 2-1 na kwenye mechi iliyofuata dhidi ya Mbao alifunga bao la ushindi katika ushindi wa 3-2,” amesema Kaburu.

Kiongozi huyo amesema kama ilivyokuwa kawaida kwa wachezaji wengine Mzamiru atazawadiwa Sh Milioni 5, ambazo zitaongeza hamasa kwa wachezaji wengine wazidi kujituma na kuipa timu yao mafanikio wanayoyahitaji.

Amesema zoezi hilo litaendelea hadi mwishoni mwa msimu na kwa msimu huu limekuwa na mafanikio makubwa kwao kwani viwango vingi vya wachezaji vilipanda kutokana na hamasa hiyo kutoka kwa uongozi.

Kaburu amesema imani yao Mzamiru na wachezaji wengine wa Simba wataitumia vizuri fursa hiyo katika mwezi mmoja uliobaki wa mechi za ligi ili kupata tuzo hiyo ya mwezi Aprili ambayo itakuwa ya mwisho kwa msimu huu wa 2016/17.


Hiyo ni mara ya pili kwa Mzamiru kubeba tuzo hiyo, huku ikiwa ni msimu wa kwanza tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.


Bofya hapa kuLike page yetu ya FB

Bofya hapa kwa habari za michezo zaidi.

Read More

Friday, 28 April 2017

SERENGETI BOYS TAYARI KWA VITA YA KESHO NA CAMEROON NCHINI HUMO.

Baada ya kukaa kwa mwezi mmoja nchini Morocco pamoja na kucheza michezo miwili ya kirafiki dhidi ya wenyeji wa Michuano ya U17 Gabon huku ikipata ushindi wa magoli 2-1 mechi zote kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania kwa jina kama Serengeti Boys usiku wa kuamkia Leo kimetua salama nchini Cameroon kwa mechi mbili za kirafiki.


Wakiongozwa na Kocha Mkuu wao Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ vijana wa Serengeti Boys wataanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa wenyeji timu ya vijana ya Cameroon utakaochezwa kesho siku ya Jumamosi ukiwa ni mchezo wa Maandalizi ya Michuano ya AFCON kwa vijana inayotarajiwa kutimua vumbi May 14 nchini Gabon.


Serengeti Boys imekuwa gumzo barani Afrika na kuanza kutabiriwa kuwa ni timu ambayo inatakiwa kuchungwa zaidi katika Michuano ya AFCO U17 inayotarajiwa kuanza mwezi wa tano kutokana na kuonesha upinzani na kuzifunga timu kubwa ambazo zipo katika michuano hiyo hii ni  baada ya kutoka sare na Ghana ya mabao 2-2 mjini Dar es salaam na kugawa dozi kwa wenyeji Gabon mechi zote mbili kwa ushindi wa maabao 2-1.


Serengeti Boys inakutana na Cameroon siku ya kesho huku ikiwa na kumbuku ya kufanya vema michezo yote ya kirafiki huku ikiwa haijawahi hata kupoteza mchezo mmoja wa kimataifa ukiachana na ule ilipofungwa na Congo-Brazaville katika hatua ya kutafuta tiketi na baada ya mchezo wa kesho timu hizo zitarudiana tena siku ya Jumanne.



Serengeti Boys inatarajia kwenda Gabon kwa ajili ya Michuano hiyo ya AFCON U17  May 7 ambapo Michuano hiyo itaanza May 14 huku Tanzania ikiwa kundi  B na timu za Ethiopia waliopewa nafasi ya Mali ambao wamefungiwa na FIFA kwa miaka minne nyingine ni Niger na Angola na Kundi A lina timu za Ghana,Cameroon,Gabon na Guine na kila kundi litatoa timu mbili ambazo moja kwa moja zitafuzu Michuano ya Kombe la Dunia kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 zitakazofanyika nchini India Novemba mwaka huu.
Read More

Thursday, 27 April 2017

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 28 Aprili 2017, atapokea Taarifa ya zoezi.

Taarifa kwa vyombo vya habari


JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS IKULU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, kesho tarehe 28 Aprili 2017, atapokea Taarifa ya zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma katika Ukumbi wa Chimwaga Mkoani Dodoma.

Taarifa hiyo itawasilishwa kwa Mheshimiwa Rais na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mheshimiwa Angellah Kairuki.

Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma liliendeshwa na Serikali kuanzia Mwezi Oktoba mwaka 2016.


Jaffar Haniu,
Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU,
Chamwino, Dodoma.

27 Aprili, 2017.
Read More

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOANI MWANZA.

  • WATU WA NNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI WILAYANI SENGEREMA.

  • MTU MMOJA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMPA UJAUZITO MJUKUU WAKE WILAYANI ILEMELA.

KWAMBA TAREHE 25.04.2017 MAJIRA YA SAA 13:40HRS KATIKA MTAA WA NYATUKALA WILAYA YA SENGEREMA MKOA WA MWANZA, WATU WA NNE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA KATIKA MAUAJI YA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA SELFU AMRI @ MANUNGWA MIAKA 71, ALIYEUAWA KWA KUPIGWA NA KITU CHENYE NCHA KALI KICHWANI KWENYE PAJI LA USO NA KUFARIKI DUNIA PAPO HAPO NA WATU WANAODAIWA KUWA NI WANAFAMILIA, KITENDO AMBACHO NI KOSA LA JINAI.



INADAIWA KUWA MAREHEMU ALIKUWA AKIISHI MWENYEWE HAPO NYUMBANI KWAKE NA SIKU YA TAREHE TAJWA HAPO JUU BAADHI YA NDUGU WALIKUA WAKIPIGA SIMU YAKE BILA MAFANIKIO, KUTOKANA NA HALI HIYO NDUGU WALIKWENDA HADI  HAPO NYUMBANI KWAKE NA KUKUTA MILANGO IKIWA IMEFUNGWA LAKINI WALIPOCHUNGULIA DIRISHA LA CHUMBANI KWAKE WALIONA MWILI WAKE UKIWA UMELALALA KITANDANI NDIPO WALITOA TAARIFA POLISI.



ASKARI WALIFIKA HADI ENEO LA TUKIO NA KUFANYA TARATIBU ZA KUINGIA NDANI NA KUUKUTA MWILI WA  MAREHEMU KITANDANI HUKU UKIWA NA JERAHA KWENYE PAJI LA USO, AIDHA BAADA YA TARATIBU ZA ENEO LA TUKIO KUFANYIKA, ASKARI WALIUCHUKUA MWILI WA MAREHEMU NA KUUPELEKA HOSPITALI YA RUFAA YA BUGANDO KWA AJILI YA UCHUNGUZI ZAIDI WA KITAALAMU.


KUTOKANA NA KIFO HICHO ASKARI WALIFANYA UPELELEZI AMBAPO WALIFANIKIWA KUWAKAMATA WATU WA NNE WANAODAIWA KUSHIRIKI KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE KATIKA KUFANIKISHA MAUAJI HAYO, KATI YAO WAPO BAADHI AMBAO WANAMAHUSIANO NA MAREHEMU LAKINI MAJINA TUNAYAHIFADHI KWA AJILI YA UCHUNGUZI, MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI, CHANZO CHA MAUAJI HAYO INADAIWA KUWA NI MGOGORO WA MIRATHI YA MALI ZA FAMILIA.



KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MWANZA, AKIWAOMBA KUACHA TABIA YA KUJICHUKULIA SHERIA MKONONI KWANI NI KOSA LA JINAI BALI PINDI WANAPOKUWA KATIKA MIGOGORO YA AINA YEYOTE ILE NA WATU WENGINE WANATAKIWA KUTOA TAARIFA KWA VYOMBO HUSIKA KAMA VILE POLISI, MAHAKAMA AU MABARAZA YA ARDHI ILI HATUA ZA KISHERIA ZIWEZE KUFUATWA NA HAKI IWEZE KUPATIKANA.
 KATIKA TUKIO LA PILI,



MNAMO TAREHE 25.04.2017 MAJIRA YA SAA 20:15HRS USIKU KATIKA MTAA WA NYASAKA KATA YA NYASAKA WILAYA YA ILEMELA JIJI NA MKOA WA MWANZA, MTU ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA KALA MACHAGE MIAKA 66, MKAZI WA MTAA WA NYASAKA ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZA KUMBAKA NA KUMPA UJAUZITO MJUKUU WAKE JINA TUNALIHIFADHI MWENYE UMRI WA MIAKA 16, MWANAFUNZI WA KIDATO CHA PILI SHULE YA SEKONDARI NYASAKA, KITENDO AMBACHO NI KINYUME NA SHERIA.


INADAIWA KUWA MTUHUMIWA ALIKUWA AKIISHI  NA MJUKUU WAKE NYUMBANI KWAKE TOKEA MWAKA 2011 AKITOKEA MUSOMA VIJIJINI, INASEMEKANA KUWA KWA KIPINDI CHOTE HICHO MTUHUMIWA ALIKUA NA TABIA YA KUMFANYIA UKATILI MJUKUU WAKE KWA KUMWINGILIA KIMWILI WAKATI AMBAPO MKEWE HAYUPO HUKU AKIMTISHIA KUWA ENDAPO ATASEMA BASI ATAMUACHISHA SHULE KISHA ATAMRUDISHA KIJIJINI KWAO.



INASEMEKANA KUWA BINTI ALIENDELEA KUVUMILIA HALI HIYO BILA KUMWAMBIA MTU YEYOTE, NDIPO TAREHE TAJWA HAPO JUU  WAALIMU WALITILIA MASHAKA HALI YAKE YA KIAFYA NDIPO WALIMPELKA  HOSPITALI KWA AJILI YA UCHUNGUZI WA DAKTARI, NDIPO BAADA YA UCHUNGUZI BINTI ALIGUNDULIKA KUWA ANAUJAUZITO WA MIEZI MINNE NA ALIPOHOJIWA ALIDAIWA KUWA AMEPEWA NA BABU YAKE.



WAALIMU WALITOA TAARIFA POLISI KUHUSIANA NA TUKIO HILO, AMBAPO ASKARI WALIFANYA UFUATILIAJI WA HARAKA NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA, MTUHUMIWA YUPO POLISI KWA MAHOJIANO PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI ILI HATUA STAHIKI ZA KISHERIA ZIWEZE KUCHUKULIWA DHIDI YAKE.



KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA ONYO KWA BAADHI YA WATU WENYE TABIA YA KUWATAMANI KIMAPENZI WANAFUNZI KWA KUWARUBUNI AIDHA KWA FEDHA ZAO KUACHA TABIA HIYO MARA MOJA, PIA ANAWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA POLISI ZA WATU WENYE TABIA ZA AINA KAMA HII ILI WAWEZE KUKAMATWA NA KUFIKISHWA KATIKA VYOMBO VYA SHERIA.



IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI

KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA
Read More

The front pages of Newspapers in Tanzania today, APRIL 27,2017.

Read More