Wednesday, 26 April 2017

MTAZAMO: Mambo 15 Mwanamke Huangalia Kabla Kukupenda.

Hebu tuseme ukweli, kuna wakati mwingine ambao wanaume wanashindwa kuwaelewa wanawake. Unaweza ukamwaproach mwanamke huku ukijua wazi hutatoboa lakini unashangazwa mwanamke kama huyo anakukubali fasta.

Na wakati mwingine utaapproach mwanamke ambaye unaamini kuwa ni rahisi kabisa kumtongoza lakini ukirusha nyavu badala ya kushika samaki inanasa mawe (sitaki kusema kinachotokea wakati mwanamke anakuzima mbele ya hadhira)

...halafu sasa kuna wale marafiki zetu ambao kila wakati wao wakitongoza wanakataliwa. (inauma sana)

Well, usitie shaka tena coz hivi karibuni kama Nesi Mapenzi tumekuwa tukitafiti kwa kuuliza wanawake ni mambo gani ambayo yanawavutia sana kutoka kwa wanaume na mambo ambayo yanaweza kuwafanya wafall in love na wanaume na haya ndio mambo ambayo waliyazungumzia sana:

  • Kuvalia nadhifu
Kulingana na wanawake ni kuwa mwanaume anapaswa kuvalia nadhifu kila wakati. Hii ni muhimu kwa mwanaume kwa kuwa huwezi kujua ni wapi au lini unaweza kukutana na mwanamke wa ndoto yako. Ni jambo muhimu la kuzingatia lakini masikitiko ni kuwa ni wanaume wachache ambao huwa wanaona umuhimu ikija katika hili swala. Ok. ni hivi, kuanzia sasa hadi milele hakikisha kuwa unavalia kisafi na kinadhifu wakati wote, jipulize marashi na utumie bidhaa zote za wanaume ambazo zitakupamba.

  • Kuwa na msimamo
Jambo ambalo wanawake wanachukizwa kutoka kwa wanaume ni kuona mwanaume ambaye hana msimamo thabiti. Mara leo anasema hivi mara siku nyingine yuko hivi. Well, hapa siongei kuhusu mwanaume ambaye mambo yake hayajulikani (mysterious) La. Naongea kuhusu wale wanaume ambao hawawezi kuwa na misimamo yao wenyewe. Akili zao haziwezi kujitegemea, hawezi kusema jambo mpaka aulize ushauri kwa wenzake ama kwa marafiki zake. So kama wewe ni mwanaume ambaye una tabia kama hizi ziache kuanzia sasa. Nataka ujeuke. Ukiwa na tabia kama hii hutatoboa katika kutongoza mwanamke.
  • Mwanaume mwenye kuvutia
Mwanaume ambaye anajua kuvutia wanawake ni silaha nzito katika sanaa ya kutongoza. Wanawake wanapenda mwanaume yeyote ambaye ana chembechembe za kusisimua wanawake. Na mwanaume kama huyu ni yule ambaye ana uwezo wa kutumia miondoko ya mwili ipasavyo, wale ambao wanajua kutumia sanaa ya kubanta, na wale wanaojua kuzungumza maneno ya kunata.

  • Mwili mzuri/shepu
Kama vile ambavyo ungependa mwanamke mwenye shepu na figa, pia wanawake wanapenda wanaume wenye shepu. So utafanyaje kama wewe una shepu la duara? Ingia gym, fanya mazoezi ya kukimbia angalau dakika 30 kila siku. Hii itakufanya uwe na toni nzuri kwa mwili wako. Si mimi ndio nimesema hivi, ni maneno kutoka vinywa vya wanawake. Anza mazoezi pindi utakapomaliza kusoma hii post.

  • Kuwa na sanaa ya ucheshi
Mwanamke anaweza kujua iwapo mwanaume anachembechembe za ucheshi au la wakati ambapo anaongea naye. Ni hivyo tu ambavyo unahitajika kuwa navyo wakati kama unataka kumfurahisha mwanamke. Kila wanawake wanajua kwamba mwanaume ambaye ni mcheshi huwa anavutia sana haswa ikija katika maswala ya kudeti na wakati wanapochat nao kupitia kwa simu. Hivyo jambo lako la kufanya ni hakikisha ya kuwa wakati unapoongea na mwanamke unamchekesha. Usijilazimishe kama wewe si mcheshi. Mwanamke anaweza kucheka kwa mizaha ambayo hata haichekeshi kama umemsoma mambo anayoyapenda.
  • Mwanaume ambaye halazimishi mambo
Mwanaume ambaye hulazimisha mambo huwa ni wanaume wanaochukiza zaidi ikija katika mchezo wa kudeti. Mwanaume wa kulazimisha ni yule ambaye anakubali kushindwa ili kuzuia mgogoro na mtu ambaye amemshinda kihadhi. Wewe kama mwanaume haupaswi kujidhalilisha mbele ya yeyote yule, hata kama ni marafiki zako. Kuwa na misimamo yako mwenyewe katika maisha yako. Kama unaona kuwa unakosewa una haki ya kupaza sauti yako usikike balada ya kukasirika ama kusinyaa.
  • Kazi nzuri na hela ndefu
Ok. Haya si maoni yangu. Ni mambo ambayo yametamkwa kutoka kwa vinywa vya wanawake. Lakini ngoja tuseme ukweli...pesa ni muhimu ikija katika maswala ya mapenzi. Ni hivi! Wewe hupenda wanawake warembo zaidi kuliko wanawake wabovu. Kweli? Hivyo hivyo wanawake hupenda wanaume ambao ni matajiri zaidi kuwaliko wale maskini. Kuwa tajiri na kuendesha gari la kifahari ni advantage kwako (usitie wasiwasi, haya ni maoni ya wanawake tu. hapa Nesi Mapenzi tushalizungumzia tatizo hili mara kwa mara, pesa si muhimu katika kutongoza, ushapu wako ndio muhimu)
  • Mwanaume ambaye anaheshimiwa na wengine
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawaheshimu, lakini pia wanapenda kuwa na wanaume ambao wanaheshimiwa na wengine. Kama kuna mtu hakuheshima, hayo ni makosa yako? Kama ni yako basi hakikisha kuwa unatatua. Lakini kama si makosa yako basi si lazima ujihusishe nao. Simama wima na utetee haki yako ya kuheshimiwa na kila mtu. Tumeelewana?
  • Mwanaume anayejiamini
Kuwa na confidence ni muhimu kwa kila mwanaume. Ni nguvu ya kuzimu ambayo kila mtu utakayekutana naye atakuonea gere. Mwanaume anayejiamini huwavutia wanawake kwa kuwa anajiamini yeye mwenyewe pamoja na uwezo wake wa kuyaona mambo jinsi yalivyo ulimwenguni.

  • Mwanaume anayeonekana vizuri
Huku ni kuanzia kule kujiweka kimwili. Vile ambavyo unasimama kama mwanaume. Je mapozi yako yakoje? Je unavalia nguo kulingana na mwili wako? Wakati unapoongea unazungumza na ishara zipi? Haya yote ni baadhi ya mambo ambayo  ni muhimu na yanayowafanya wanawake wakutambue kama wewe ni mwanaume bora wa kumchumbia au la.

  • Mwanaume anayejua kuzungumza
Kama tu vile kujua jinsi ya kutumia ucheshi katika mazungumzo yako, kujua jinsi ya kuzungumza na mwanamke kwa kutumia Sanaa ya Mazungumzo kama vile banta, miondoko ya mwili na kuchanganya Programu ya Isimu Ubongo ni muhimu zaidi kwa kuwa kutamfanya mwanamke kujiskia huru zaidi akiwa na wewe na ni mambo ambayo mwanamke anatamani kutoka kwa mwanaume yeyote.

  • Tabia ya kuheshimu
Kuwa na tabia ya kuheshimu wengine vile inavyotakikana. Wanawake wote wazuri hawawapendi wanaume ambao wanapenda kuwachukulia vibaya wengine. Usiwe mbaya kwa watu walioko chini yako bila ya kuwa na sababu yeyote. Ukiheshimu wengine nao pia watakuheshimu. Wanawake huwaona wanaume wenye tabia ya kuwaheshimu wengine kuwa wanaweza kuwa wazazi wazuri. So hakikisha kuwa unatabia nzuri wakati wote.

  • Kuwa mwanaume alpha
Wanawake wazuri huwa kwa mikono mwa wanaume bora. Hakuna mwanamke atataka kuwa na mwanaume mwoga, asiyejiamini, asiyeheshimu wengine. Itakuwa ushawahi kugundua kitu flani, kwa kawaida huwa kuna mwanaume mmoja katika kikundi flani ambapo yeye anadeti wanawake warembo zaidi ilhali wenzake wanadeti wanawake wa kawaida.

  • Mfanye ajihisi huru
Wanawake wanapenda wanaume ambao wanawafanya wajihisi huru wakiwa nao. Hii ni kulingana na usemi kutoka kwa wanawake. Hivyo kama wewe unakuwa na tabia za maswali yasioisha, ukali, woga ama kutojiamini basi utamfanya mwanamke ashindwe kujiskia comfortable akiwa na wewe. Jambo la kuhakikisha ni kuwa unautoa wasiwasi wowote ambao unaweza kujitokeza wakati unapoongea na yeye.

  • Mwanaume mwenye usambamba/ compatibility
Ok. Tatizo kuu linajitokeza hapa. Mara nyingi mwanaume anaweza kumpendeza mwanamke kwa kila kitu lakini mwanamke anaweza asikubali mwitikio wako kwa kuwa hamna uwiano ulio sawa. Mwanamke anaweza kukukataa kwa sababu zake binafsi. Kama unataka kufanikiwa na hili basi hakikisha kuwa unakuwa mkweli, makinika na interests zake na usome mambo anayopenda na kuchukia. Kama ataona kuwa kuna uwiano ndani yenu, basi ni rahisi kwa yeye kukukubali.



Read More

HIMID MAO: Tuna morali kubwa ya kupata matokeo mazuri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho (ASFS) dhidi ya Simba.


NAHODHA Msaidizi wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Himid Mao ‘Ninja’, ameweka wazi kuwa wana morali kubwa ya kupata matokeo mazuri kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Sports) dhidi ya Simba Jumamosi ijayo.

Kikosi cha Azam FC kipo kwenye maandalizi makali kuelekea mchezo huo, ambapo tayari kimeshaingia kambini tokea jana katika makao makuu ya klabu hiyo ndani ya viunga vya Azam Complex kujiandaa na mchezo.

Himid ameuambia mtandao rasmi wa klabu www.azamfc.co.tz kuwa kikosi hicho kipo vizuri na watanufaika na urejeo wa wachezaji wao muhimu waliokuwa majeruhi.

“Morali iko juu, timu ipo vizuri bahati nzuri wachezaji wenzetu karibia asilimia 90 wapo vizuri na wapo fiti na wako tayari kwa mchezo na naamini kocha atakuwa na nafasi nzuri ya kuchagua timu yake ya kwenda kucheza mchezo huo,” alisema.

Kiungo huyo anayesifika kwa ukabaji na mwenye mashuti makali, aliongeza kuwa mchezo huo utakuwa mgumu licha ya kufanikiwa kuwafunga mara mbili katika mechi mbili zilizopita.

“Usidhani kama mchezo huu wa tatu utakuwa mrahisi kama mara mbili zilizopita tulizoshinda, kwani Simba nayo inajipanga, lakini naamini sisi tutajipanga vizuri zaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo inayokuja,” alisema.


Himid ambaye amekulia kwenye timu hiyo kwa takribani miaka tisa sasa, alitoa wito kwa mashabiki wa Azam FC kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo ili kuwapa sapoti kwani wao ni sehemu muhimu sana katika timu na uwepo wao utawaongezea nguvu zaidi uwanjani ya kuibuka kidedea.


Bofya hapa kuLike page yetu ya FB

Bofya hapa kwa habari za michezo zaidi.
Read More

Jamhuri imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi ya jijini Arusha kuiondoa kesi ya kujifanya Afisa usalama wa Taifa.


Upande wa Jamhuri imeiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi  ya jijini Arusha kuiondoa kesi ya kujifanya Afisa usalama wa Taifa na kujipatia chakula  katika hotel moja ya kimataifa jijini Arusha inayomkabili aliyekuwa Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa huo  Bw. Lengai

Akitoa ombi hilo Wakili wa Serikali Bi. Grace Madikenya mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Hakimu mkazi Arusha, Mhe. Gwantwa Mwakuga, alisema upande wa Jamhuri hauna nia ya kuendelea na kesi hiyo sababu shahidi mmoja muhimu yupo nje ya nchi kwa miezi 18. 
 
 “Sasa tumeona tutamtesa mteja wetu. Hivyo kwa nia njema kabisa tumeamua kuiondoa mahakamani kesi hii, maana miezi hii 18 ni  mwaka mmoja na miezi sita,”alisema. 
 
 Ombi hilo lilipingwa vikali na Wakili wa utetezi, Bi. Edna Haraka na kuiomba mahakama hiyo iendelee na kesi hiyo, kwa madai kuwa upande wa mwendesha mashitaka unatumia Mahakama kama kichaka cha kumnyima haki mteja wao na kumnyanyasa. 
 
Alisema upande huo hauna nia njema na mshitakiwa na kwamba kitendo cha kuiondoa kesi hiyo mahakamani sio mara ya kwanza ni mara ya pili, ambapo ya kwanza waliomba hivyo na mahakama ilipofuta walimkamata mteja wao na kumnyima dhamana. 
 
“Sasa leo tupo katika kusikiliza shahidi wa tatu na badala ya kuleta shahidi walileta maelezo ya shahidi na leo wanakuja na stori ya kuiondoa ili waendelee kumyanyasa mteja wetu. Hapana! Ofisi hiyo ya Mwanasheria Mkuu inatumika vibaya kwa kivuli cha Mahakama,”alisema Edna
 
Wakili huyo alisema serikali ya sasa inasisitiza mpango wa kuharakisha mashauri kusikiliza wa BRN, sasa wakati inafanyika hivyo wengine wanachelewesha kwa sababu zao. 

Hakimu Gwantwa Mwakuga baada ya kusikiliza pande zote mbili, alisema atatoa uamuzi Aprili 28 mwaka huu, ya  kama anakubali shauri liondolewe au la. 


Bw.  Lengai anakabiliwa na shitaka la kujifanya Afisa Usalama wa Taifa na kujipatia huduma ya chakula na malazi kwenye Hotel ya kimataifa ya Highway ya jijini Arusha.


Read More

Tuesday, 25 April 2017

Kocha Mkuu wa timu ya Toto African amesema timu hiyo kamwe haitashuka daraja.


Kocha  Mkuu wa timu ya  Toto African ya Jijini Mwanza maarufu wanakisha mapanda,  Furgence Novatus amesema  timu hiyo kamwe  haitashuka daraja  kutokana na matumaini makubwa ya ushindi kwa mechi nne  walizobakiza licha ya kuwa wako katika mstali wa hatari kushuka ligi.

Kocha huyo ametoa tambo zake mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki kati ya Toto African na Buselesele FC, mabingwa wapya wa Mkoa wa Geita ligi daraja la tatu, ambapo Novatus amesema hata Mabingwa wa ligi kuu timu ya Yanga hawatawabakisha salama wasipojipanga na kwamba hakuna urafiki katika hatua waliopo.
Baada ya mchezo huo ambao timu hizo zilitoshana nguvu, wadau wa soka Mkoani Geita wamekuwa na matumaini makubwa na timu yao, ambayo iko katika maandalizi ya kuchuana ligi daraja la pili.


Diwani wa kata ya Buselesele Godfrey Miti ambaye ni mdhamini wa Timu ya Buselesele FC amedai kuwa matumaini makubwa aliyonayo ni kuakikisha timu hiyo inafikia kiwango cha ligi kuu na kwamba yeye pamoja na wadau wa mpira Mkoani Geita hataakikisha timu hiyo inapanda daraja.
Read More

The front pages of Newspapers in Tanzania today, APRIL 25,2017































Read More

Sunday, 23 April 2017

Breaking Newz: Haji Manara kufungiwa miezi 12.




Kamati ya Nidhamu ya TFF, imetangaza kumfungia miezi 12 Msemaji wa Simba, Haji Manara.Pia nakulipa faini ya Shilingi  milioni 9.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Nidhamu ya TFF, Wakili Jerome Msem
wa amesema Manara amefungiwa miezi 12 kutokana na utovu wa nidhamu.

Akizungumza na waandishi wa habari hivi punde, 

Kosa la kwanza kuzungumzia ukabila na chuzi za namna ya kitendo alichokifanya.

kuwa kanuni imemuadhibu mlalamikiwa kwa kosa lake kwa mujibu wa kanuni la 53 (1,2) katika kanuni za nidhamu za TFF.

Msemwa amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya kubaini Manara amefanya utovu mkubwa wa nidhamu.
Read More

Thursday, 20 April 2017

TODAY'S NEWSPAPERS THURSDAY APRIL 20,2017.



Read More