Nifate Twitter
Home
All posts
Friday, 30 June 2017
Thursday, 29 June 2017
Baada Donald Ngoma kuongeza mkataba wa kuichezea Yanga.
Baada ya mshambuliaji Donald Ngoma, kuongeza mkataba wa miaka miwili kuichezea Yanga, kocha mkuu wa timu hiyo George Lwandamina, amesema kitu alichokifanya Ngoma ni cha kupongezwa.
Lwandamina ameiambia Goal, anamuhitaji sana Ngoma kwenye kikosi chake cha msimu ujao hivyo kitendo cha kuongeza mkataba kimempa matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao.
“Ni jambo zuri na wachezaji wengine wanatakiwa kuiga mfano wake Ngoma ni mchezaji anayestaili kuichezea Yanga kutokana na rekodi yake aliyoifanya akiwa na timu hiyo huko nyuma,”amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema baada ya kushindwa kumtumia kwa muda mrefu msimu uliopita anaamini msimu ujao atakuwa na nafasi kubwa ya kutimiza majukumu yake uwanjani na kuwafurahisha mashabiki wao.
Amesema kubaki kwa Ngoma kwenye kikosi cha Yanga kutaongeza hofu hata kwa wapinzani wao, na kuendelea kuiogopa timu hiyo msimu ujao.
“Kuwa na Ngoma tunapata uhakika wa kuogopwa na wapinzani wetu kwani wamekuwa wakimuhofia sana hiyo ni faida kwetu ambayo tunapaswa kuitumia vyema kupata pointi tatu,”amesema.
Ngoma amesaini Yanga, mkataba wa miaka miwili, na kuzima uvumi ambao ulikuwa umeenea kuwa yupo mbioni kujiunga na wapinzani wao Simba ambao nao walikuwa wanamuhitaji.
Mzimbabwe huyo ameigarimu Yanga dola 420,000 kwa ajili ya mkataba huo utakaomuweka Jangwani hadi mwishoni mwa msimu wa 2019.
Lwandamina ameiambia Goal, anamuhitaji sana Ngoma kwenye kikosi chake cha msimu ujao hivyo kitendo cha kuongeza mkataba kimempa matumaini ya kufanya vizuri msimu ujao.
“Ni jambo zuri na wachezaji wengine wanatakiwa kuiga mfano wake Ngoma ni mchezaji anayestaili kuichezea Yanga kutokana na rekodi yake aliyoifanya akiwa na timu hiyo huko nyuma,”amesema Lwandamina.
Mzambia huyo amesema baada ya kushindwa kumtumia kwa muda mrefu msimu uliopita anaamini msimu ujao atakuwa na nafasi kubwa ya kutimiza majukumu yake uwanjani na kuwafurahisha mashabiki wao.
Amesema kubaki kwa Ngoma kwenye kikosi cha Yanga kutaongeza hofu hata kwa wapinzani wao, na kuendelea kuiogopa timu hiyo msimu ujao.
“Kuwa na Ngoma tunapata uhakika wa kuogopwa na wapinzani wetu kwani wamekuwa wakimuhofia sana hiyo ni faida kwetu ambayo tunapaswa kuitumia vyema kupata pointi tatu,”amesema.
Ngoma amesaini Yanga, mkataba wa miaka miwili, na kuzima uvumi ambao ulikuwa umeenea kuwa yupo mbioni kujiunga na wapinzani wao Simba ambao nao walikuwa wanamuhitaji.
Mzimbabwe huyo ameigarimu Yanga dola 420,000 kwa ajili ya mkataba huo utakaomuweka Jangwani hadi mwishoni mwa msimu wa 2019.
Wednesday, 28 June 2017
Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF na Katibu Mkuu wake wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Rais
wa Shirikisho la Soka nchini, Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake,
Selestine Mwesigwa wanashikiriwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU) na wapo katika Kituo cha Polisi Salander Bridge ili
kupisha uchunguzi dhidi yao.
Tukio
hilo limethibitishwa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Takukuru,
Mussa Misalaba alipokuwa akihojiwa na kituo cha Radio EFM leo. Misalaba
amesema ni kweli wanawashikilia na taarifa zaidi wataitoa baada ya
kumaliza uchunguzi wao.
Licha
ya kuwa tuhuma zinazowakabili hazijawekwa wazi, lakini mwezi uliopita
ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iliripoti
kuhusu mabilioni ya shilingi yaliyobainika kuchotwa kwenye akaunti za
TFF na kulipwa kwa wadau wa soka kinyume cha sheria.
Miongoni mwa waliotuhumiwa kunufaika na fedha hizo ni Rais wa TFF, Jamal Malinzi na aliyekuwa msaidizi wake, Juma Matandika.
Wengine
ni aliyekuwa katibu mkuu wa kilichokuwa Chama cha Soka (FAT sasa TFF),
Michael Wambura na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Ayubu Nyenzi.
Gazeti
la Nipashe lilieleza kubaini kuwa, mkutano mkuu wa wanachama wa TFF
uliofanyika Desemba 2011 uliidhinisha Kampuni ya Ukaguzi ya TAC kuwa
mkaguzi wa hesabu za shirikisho kwa miaka mitano kuanzia mwaka ulioishia
Desemba 31, 2011.
Ripoti ya ukaguzi wa kampuni hiyo inaonesha
kuwa, katika kipindi cha kuanzia Agosti 15, 2014 hadi Septemba 30, 2015,
TFF ililipa jumla ya Sh. milioni 274.072 kwa Wambura na kampuni za
Punchlines (T) Ltd na Artriums Dar Hotel Ltd bila kuwa na nyaraka
stahiki.
Pia, ripoti ya ukaguzi maalum wa fedha za udhamini wa
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kwa timu ya taifa (Taifa Stars)
iliyotolewa Oktoba 2, 2014, inabainisha matumizi mabaya ya mabilioni ya
shilingi miongoni mwa baadhi ya watendaji wa TFF.
Katika ripoti
hiyo inaelezwa kuwa, kuanzia Novemba 13, 2013 hadi Februari 15, 2014,
jumla ya dola za Marekani 315,577 (sawa na sh. milioni 688.368)
zilichotwa kwenye akaunti ya fedha za udhamini wa TBL kwa Taifa Stars na
kutumika kinyume cha makubaliano yaliyomo kwenye mkataba wa shirikisho
na kampuni hiyo.
Inaelezwa pia kwenye ripoti hiyo kuwa kuanzia
Novemba 11, 2013 hadi Machi 11, 2014, jumla ya dola za Marekani 381,248
(Sh. milioni 831.616) zilichotwa kwenye akaunti hiyo na kutumika kwa
shughuli ambazo hazijaanishwa katika mkataba wa TBL na TFF.
Miongoni
mwa waliotajwa kwenye ripoti hiyo kutumia kinyume fedha hizo ni
Malinzi, Matandika, Ali Ruvu, Nyenzi, Ally Mayay, Chama cha Soka Mkoa wa
Mtwara, Chama cha Soka Mkoa wa Mbeya na aliyekuwa kocha wa Taifa Stars,
Kim Poulsen.
Ripoti ya ukaguzi wa TAC inaonesha Wambura alilipwa
jumla ya Sh. milioni 67.5, Punchline (T) Ltd ililipwa Sh. milioni
147.154 na Artriums Dar Hotel Ltd ililipwa Dola za Marekani 28,027 (Sh.
milioni 59.417).
Aidha, ripoti hiyo inaonesha malipo ya maelfu
hayo ya Dola kwa Artrium yalifanyika siku moja ya Machi 4, 2015 kwa TFF
kuandika vocha nne zenye namba 001467, 001468, 001469 na 001470, tatu
zikiidhinisha malipo ya Dola 9,000 kila moja wakati moja ikiidhinisha
malipo ya Dola 1,027.
Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa timu ya
ukaguzi ilibaini malipo kwa wadau hao wa soka yalifanyika bila idhini ya
Kamati ya Utendaji ya TFF.
Tuesday, 27 June 2017
Donald Ngoma imeaminika ameamua kuachana na soka la Bongo.... Aitema SIMBA NA YANGA.
Donald Ngoma inaaminika ameamua kuachana na soka la
Bongo, badala yake anatimkia Afrika Kusini atakapojiunga na Polokwane
alikosaini miaka mitatu.
Wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe Donald Ngoma, akitarajiwa
kuwasili nchini leo kumalizana na ama klabu ya Yanga au mahasimu wao
Simba, mchezaji huyo ni kama anachezea akili za miamba hao wa soka baada
ya taarifa za ndani kudai ameshasaini mkataba wa miaka mitatu kuichezea
timu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi Kuu nchini Afrika Kusini.
Ngoma alitarajiwa kuwasili Dar es Salaam, leo kwa ajili ya kuongeza
mkataba wa kuendelea kuichezea Yanga, lakini pia mshambuliaji huyo
alishafanya mazungumzo ya awali na viongozi wa Simba na inasemekana ujio
wake ilikuwa ni kwa ajili ya kukamilisha usajili wake kwa kusaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Kwa mujibu wa Mtandao wa KickOff.com, imethibitika
Mzimababwe huyo amekamilisha zoezi lake la usajili kwenye klabu hiyo,
baada ya kuwa huru kufuatia kumaliza mkataba wake wa miaka miwili na
mabingwa wa soka Tanzania Yanga.
Taarifa hiyo imesema Ngoma, alisaini mkataba huo wa miaka mitatu
baada ya kufuzu vipimo vya afya na anatarajiwa kujiunga na miamba hao wa
ligi ya ABSA,ambao kwa sasa wanashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa
ligi hiyo.
Akiwa Polokwane City, Ngoma anatarajiwa kukutana na Mzimbabwe mwezake
ambaye pia anacheza nafasi ya George Chigova aliyewahi kucheza naye FC
Platinum chini ya kocha Norman Mapeza.
BOFYA HAPA KUJUA VIINGILIO VYA KWENYE MAONYESHO YA UWANJA WA SABASABA MWAKA HUU
BOFYA HAPA KUJUA VIINGILIO VYA KWENYE MAONYESHO YA UWANJA WA SABASABA MWAKA HUU
Subscribe to:
Posts (Atom)
Sosial Media
Navigation List
Paling Dibaca
-
Nilipokuwa natoa mada kuhusu miaka 50 ya Azimio la Arusha niliongelea pia suala la umakini wa viongozi katika kauli zao. Kwamba Kiongo...
-
Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli ameagiza msanii Emmanuel Elibariki anayejulikana kama Nay wa mitego kuachiliwa huru ma wimbo ...
-
The captain of the national team who is also an international striker who play on Club KRC GENK in the Belgium Mbwana Samatta recently...
-
BOFYA HAPA KUSOMA RATIBA YA PREMIER LEAGUE (EPL) 2017 - 2018. Haya hapa Majina ya vyuo vilivyozuiwa na TCU kuandikisha wanafunz...
-
TANZANIA IMEFUZU ROBO FAINALI KATIKA MASHINDANO YA COSAFA. AMIS TAMBWE AONGEZA MKAT...
-
Rais Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo amepokea hati ya utambulisho ya mabalozi watano walioteuliwa kuziwakilisha nchi zao hapa nchini. ...
-
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI HALMASHAURI YA WILAYA YA MAKETE Mkurugenzi Mtendaji (W)Makete kupitia kibali cha ajira mbadala kilichotole...
-
Mshambuliaji machachari wa Timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, Yohana Nkomola, amegoma kujiunga na vilabu vya ndani y...
-
Bofya hapa kupata habari mbalimbali za ndani na nje ya nchi. BOFYA HAPA KULIKE PAGE YETU YA Facebook KWA HABARI MBALIMBAL...
Kategori
Formulir Kontak
copyright© 2016. Powered by Blogger.











































